Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Karibu wiki mbili zimepita tangu mapinduzi yafanyike nchini Niger wanaume wawili wanatoa madai kinzani

Tuliyonayo asubuhi hii:

Karibu wiki mbili zimepita tangu mapinduzi yafanyike nchini Niger wanaume wawili wanatoa madai kinzani ya kuhodhi madaraka wamekuwa kimya katika siku za karibuni. Moja ni rais aliepinduliwa, ambaye alisema wiki iliyopita kwamba anashikiliwa mateka na amekuwa kimya tangu wakati huo. Mwingine ndiye kiongozi wa kijeshi anaedai kuwa alifanya mapinduzi kutokana na wasiwasi juu ya usalama wa taifa, na amewahimiza Waniger kuilinda dhidi ya uingiliaji wowote wa kigeni. Tunawaangazia viongozi hao wawili – Rais aliendolewa Mohamed Bazoum, na kiongozi wa mapinduzi Abdarahamane Tchiani.

Faustine-Archange Touadera, anaetazamiwa kuwania muhula wa tatu kama Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya wapiga kura kupitisha kwa wingi rasimu ya katiba mpya, anajinasibu kama gundi inayowaunganisha watu katika mojawapo ya nchi zenye machafuko zaidi duniani. Hata hivyo, wakosoaji wake wanamuita Touadera kama “Rais Wagner” kutokana na utegemezi wake kwa Urusi na kundi la mamluki la Wagner.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati Kanisa Katoliki na lile la Kiprotestanti yakipendekeza tume yao ya pamoja kukagua daftari la uchaguzi, tume huru ya uchaguzi, CENI, imetupilia mbali pendekezo hilo. Yaani CENI imekataa kufungua mlango kwa ukaguzi mwingine wakati mchakato wa uchaguzi ukiendelea na kalenda ya uchaguzi lazima kuheshimiwa. Tume hiyo ya uchaguzi imeelezea mshangao wake kuona makanisa hayo mawili, badala ya kuwa katikati yanaegemea upande wa upinzani.

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistani Imran Khan sasa ni mfungwa katika gereza lenye ulinzi mkali, baada ya mahakama siku ya Jumamosi kumtia hatiani kwa kosa la rushwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela. Je, ni nini mustakabali wa Imran Khan katika siasa baada ya kukamatwa ?

Jamii ya Wahadzabe ni moja kati ya makabila yaliyobaki duniani yanayoendeleza shughuli za uwindaji, na inadhaniwa kwamba jamii hiyo imeishi kaskazini mwa Tanzania, ikila matunda, mizizi na aina mbalimbali za wanyama kwa miaka zaidi ya elfu elfu 40.

Source: @dw_kiswahili

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.