Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia suluhu Hassan ametoa rambirambi ya Tsh. milioni 10 na msaada wa vyakula kwa Familia ya Mzee Msuya

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia suluhu Hassan ametoa rambirambi ya Tsh. milioni 10 na msaada wa vyakula kwa Familia ya Mzee Msuya iliyopoteza Ndugu wanne wa Familia moja usiku wa kuamkia August 03,2023 baada ya gari (Toyota Prado) walilokuwa wamepanda wakitokea Dar es salaam kwenda Same, Kilimanjaro kugongana uso kwa uso na Scania lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es salaam Wilayani Chalinze Mkoani Pwani.

Akimwakilisha Rais Samia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amekabidhi fedha, vitenge na vyakula ikiwemo mchele kilo 200, maharage kilo 100, sukari kilo 100, ngano kilo 100, mafuta,tambi ,soda maziwa na maji.

“Rais ametuelekeza tuje na vitenge ambavyo tutamfunika Mama pamoja na baadhi ya Wajukuu lakini zaidi pia na upande wa Mama zetu Wakwe ili angalau kuleta ile faraja kwamba Mh. Rais amelia msiba pamoja na nyinyi”

“Mhe Rais ametoa neno la faraja na hapa Mzee wetu Msuya kama jana alivyoahidi kwamba kwanza inatakiwa mnapotaka kupata matibabu katika hizo Hospitali kubwa ikiwemo Muhimbili na JKCI, Benjamin Mkapa Hosp. kusiwe kuna usumbufu wa aina yoyote”
Via;MillardAyoUPDATES

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.