Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tafiti: Matumizi ya dawa za tatizo la Acid Reflux kwa Muda mrefu huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu(Dementia)

Tafiti zinaonyesha Matumizi ya dawa za kutibu tatizo la Tindikali kupanda kutoka tumboni(Acid Reflux) kwa Muda mrefu huongeza hatari ya Mtu kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu(Dementia).

Utafiti huo mpya umeonyesha ukitumia baadhi ya dawa za kutibu tatizo hili la acid reflux kwa muda mrefu zaidi unakuwa kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu”dementia” kwa asilimia 33%.

Utafiti huu ulionyesha kuna uhusiano wa karibu sana kati ya matumizi ya baadhi ya dawa Kwa mgonjwa mwenye tatizo la acid reflux na kuongeza hatari ya kupata tatizo la kupoteza kumbukumbu,

Na Watu ambao hutumia dawa jamii ya proton pump inhibitors zaidi ya miaka minne(4) na Nusu walionekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi,

Ingawa utafiti huo ulishindwa kuthibitisha ni jinsi gani dawa jamii ya proton pump inhibitors(PPIs) husababisha kupungua kwa uwezo wa utambuzi-Cognitive decline.

Wataalamu wanabainisha kuwa inaweza kuwa bahati mbaya kwa kuwa watu wazee wana uwezekano mkubwa wa kutumia PPIs,

Ingawa, wanasema kuna njia mbadala kadhaa za kutumia PPIs kwa wale ambao wana wasiwasi juu ya hatari au madhara.

Utafiti huu ambao ulichapishwa August 9, 2023 kwenye jarida la Neurology linalojulikana kama “the medical journal of the American Academy of Neurology”;

ulionyesha kwamba, dawa zinazotumika sana kwa watu wenye tatizo la acid reflux ambazo ni jamii ya “proton pump inhibitors” (PPIs) zina uhusiano wa karibu na kuongeza hatari ya mtu kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu yaani dementia,

Na uhusiano huo ulionekana kwa watu ambao walitumia dawa hizo kwa muda wa Miaka minne(4) na nusu au Zaidi.

Dawa hizo jamii ya PPIs ni pamoja na;

  • omeprazole (Prilosec)
  • esomeprazole (Nexium)
  • lansoprazole (Prevacid)

Dawa hizi hufanya kazi kwa kusababisha Seli zinazotengeneza acid tumboni kupunguza kiwango cha Acid zinachozalisha.

KUMBUKA; Waandishi wa utafiti huu wanatukumbusha kwamba, Utafiti huu haujathibitisha kwamba dawa jamii ya PPIs husababisha moja kwa moja ugonjwa wa dementia,

ila ulionyesha tu kwamba,kuna Uhusiano flani kati ya hivi vitu viwili.

Ugonjwa wa Dementia ni ugonjwa ambao husababisha mtu kupoteza kumbukumbu, ugonjwa huu ni kama Alzheimer’s disease ambapo mabadiliko yasiyoyakawaida hutokea kwenye Ubongo na kuathiri uwezo wa mtu kufikiri,

Ugonjwa huu wa dementia huweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo kuathiri kabsa uwezo wa mtu kufanya kazi zake za kila siku.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.