Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

SABABU ZA VIFO VYA WATOTO WACHANGA TANZANIA NA NJE YA TANZANIA

Zipo sababu mbali mbali ambazo husababisha tatizo la vifo kwa watoto wachanga mpaka watoto wanapofikia umri wa miaka 5, Ingawa sababu hizi huweza kutofautiana kati ya Nchi moja na nyingine ila zipo sababu ambazo ni kubwa duniani pote,na sababu hizo ndyo tunazozichambua katika makala hii.

SABABU ZA VIFO KWA WATOTO WACHANGA TANZANIA NA NJE YA TANZANIA NI PAMOJA NA;

– Mtoto kupata maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria n.k

– Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati yaani premature birth, watoto hawa huwa na uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha kwasababu ya mfumo wao wa kinga ya mwili haujakamilika vizuri na kuwa imara dhidi ya mashambulizi ya magonjwa mbali mbali,hivo kuwa rahisi kushambuliwa na kila aina ya ugonjwa kama vile pneumonia,sepsis,meningitis n.k, na kupelekea mtoto kupoteza maisha

– Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,mfano mtoto kuzaliwa na uzito wa chini ya Kilogram 2.5, watoto hawa huweza kupoteza maisha kwa haraka kutokana na viungo mbali mbali vya mwili kutokukomaa hivo kupelekea matatizo kama vile kushindwa kupumua au tatizo la Intraventricular hemorrhage

– Mtoto kuzaliwa na tatizo la kukosa hewa ya oxygen kwenye ubongo(birth asphyxia),kushindwa kupumua au matatizo mengine yanayohusu mfumo wa upumuaji

– Mtoto kuzaliwa na kupatwa na tatizo la homa ya manjano au Neonatal jaundice

– Mtoto kuzaliwa na matatizo mbali mbali ya kimaumbile, matatizo ya ubongo n.k, hali ambayo huweza kupelekea viungo vya mwili kushindwa kufanya kazi vizuri,mtoto kushindwa kupumua,kukosa hewa ya kutosha na kupoteza maisha

– Mtoto kupatwa na matatizo mbali mbali wakati wa kuzaliwa kama vile; mtoto kunywa maji ya uzazi,mtoto kunyongwa na cord, mtoto kudondoka chini ya sakafu wakati mama anajifungua n.k

– Matatizo kwa mama wakati wa ujauzito kama vile; tatizo la presha kuwa juu sana wakati wa ujauzito,tatizo la kifafa cha mimba,tatizo la mlango wa mji wa mimba kushindwa kuhimili ujauzito uliobebwa yaani incompetent cervix n.k

– Matatizo mbali mbali kwenye kondo la nyuma yaani placenta,ikiwa ni pamoja na; kondo la nyuma kuachia sehemu lilipojishikiza yaani placenta abruption, kondo la nyuma kushuka chini zaidi yaani placenta praevia n.k

– Tatizo la vifo vya gafla kwa watoto ambapo kitaalam hujulikana kama sudden infant death syndrome(SIDS), hapa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo huweza kugundulika kama chanzo cha kifo kwa mtoto husika, ila baadhi ya wataalam wa afya husema kwamba tatizo la vifo vya gafla kwa watoto huweza kusababishwa na tatizo la hitilafu kwenye sehemu ya ubongo wa mtoto ambayo huhusika na kurekebisha maswala ya upumuaji kwa mtoto

VIFO KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 5, KWA ASILIMIA KUBWA HUWEZA KUCHANGIWA NA;

• Tatizo la pneumonia

• Tatizo la mtoto kuharisha sana

• Mtoto kuzaliwa na matatizo mbali mbali ya kiuumbaji yaani birth defects

• Ugonjwa wa Malaria

• Na kushambuliwa na magonjwa mengine mengi kwa urahisi kutokana na mtoto kuwa na tatizo la utapiamlo yaani Malnutrition.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.