Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Somalia yapiga marufuku  mtandao wa TikTok na Telegram

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Somalia imewaamuru watoa huduma za intaneti nchini humo kuzima uwezo wa kufikia kampuni za mitandao ya kijamii za TikTok, Telegram, na tovuti ya kamari ya 1xBet.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Jama Hassan Khalif, alitoa agizo hilo katika taarifa yake aliyoitoa Jumapili, Agosti 20, akitaja sababu za usalama na kupambana na ugaidi kuwa ni sababu za kuzizuia kampuni hizo.

Pia alitaja athari mbaya inayodaiwa kuwa ya majukwaa katika maisha ya vijana wa Kisomali.

Khalif alisema Somalia imetumia marufuku hiyo yenye utata ili “kulinda tabia ya kimaadili ya jamii ya Somalia wakati wa kutumia zana za mawasiliano na mtandao.”

Taarifa hiyo ilisomeka kwa sehemu;

“Katika jitihada za kuharakisha vita na kutokomeza magaidi ambao wamemwaga damu za watu wa Somalia, waziri wa mawasiliano na teknolojia anaagiza makampuni yanayotoa huduma za mtandao kusitisha huduma za mitandao ya TikTok, Telegram pamoja na tovuti ya kamari ya 1XBET”.

“In a bid to accelerate the war and elimination of the terrorists who have shed the blood of the Somali people, the minister of communication and technology instructs companies that provide internet services to suspend TikTok, Telegram, and 1XBET betting applications, which terrorists and groups responsible for spreading immorality use to spread graphic clips, photos and mislead society.”

Kutokana na Taarifa hiyo inaelezwa; Upatikanaji rahisi wa majukwaa haya umesababisha kuongezeka kwa matumizi dhidi ya idadi kubwa ya vijana, na kuibua wasiwasi juu ya uwezekano wa ushawishi mbaya na unyonyaji.

Hata hivo,Bunge la Kitaifa la Kenya kwa sasa linakagua ombi la kutaka kupigwa marufuku kwa TikTok kwa sababu ya ukosefu wa udhibiti wa kutosha na wasiwasi kuhusu maudhui machafu.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.