Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Hakuna Mwenye Misuli na ubavu wa Kuligawa au Kuuza Taifa hili -Rais Samia

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu amesema aliamua kunyamaza na anaendelea kukaa kimya lakini amewahakikishia Watanzania kuwa hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa la Tanzania na wala hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuiuza Nchi ya Tanzania.

Rais Samia amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika Chuo cha Tumaini Makumira, Arusha leo August 21,2023.

Rais Samia amenukuliwa akisema “Ndugu zangu, na hususani Baba Askofu Shoo, Kaka yangu Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, nimeyasikia yote uliyoyasema kuhusu usalama, amani, umoja na mwendelezo wa Taifa letu, niliamua kunyazama kimya na naendelea kunyama kimya, ninachotaka kuwahakikishia hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa hili, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuuza Taifa hili”

“Hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama tuliojenga kwenye Taifa hili, hayo itoshe kuwa ni ujumbe wangu kwenu, asanteni sana”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.