Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Nyumba iliyojengwa kwa mbao ya miaka 100 yanusurika kuteketea kwa Moto Maui- Marekekani

Nyumba iliyoezekwa kwa paa jekundu huko Lahaina bado imesimama huku mtaa unaoizunguka ukiwa umeteketea na kuwa kifusi na majivu.

Wamiliki wa nyumba hii wanasema wanahisi “wenye hatia” kwamba nyumba yao, ambayo imejengwa kwa mbao na ina umri wa angalau miaka 100, imetoka bila hata kuguswa.

“Ni nyumba ya mbao 100%, kwa hivyo sio kama tuliizuia moto au chochote,” Dora Atwater Millikin aliambia Los Angeles Times.

Bw Millikin na mkewe walisema hawana uhakika ni nini hasa kiliokoa nyumba yao ambapo walinunuakutoka kwa mtunza hesabu wa wafanyikazi wa shamba la sukari.

Bw Millikin na mkewe walikuwa safarini mkasa huo wa moto ulipozuka na wanasema kuwa nyumba hiyo ilikuwa mbovu, hivyo walitaka kuirejesha katika ubora wake.

Huenda ukarabati huo ndio uliookoa nyumba hiyo.

Walibadilisha paa la lami la nyumba na kuweka mabati yenye-kipimo vizito, wakaizungushia nyumba kwa mawe ya mto na kuondoa miti maua na majani yaliyokuwa yameizunguka.

Lakini hakuna hata moja ya vitendo hivi vilivyokusudiwa kuzima moto, walisema.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.