Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Sha’Carri Richardson ;Mwanamke Mwenye mbio Zaidi Duniani

Mmarekani Sha’Carri Richardson ametangazwa kuwa bingwa wa dunia wa mbio za masafa mafupi za mita mia moja kwa upande wa wanawake kwenye mashindano ya dunia huko Budapest.

Richardson, akishiriki fainali yake ya kwanza kuu akiwa na umri wa miaka 23, aliweka rekodi ya mashindano hayo kwa kuandikisha muda wa sekunde 10.65 na kutwaa medali ya dhahabu.

Shericka Jackson wa Jamaica alitwaa medali ya fedha huku bingwa mara tano Shelly-Ann Fraser-Pryce akiridhika na medali ya shaba.

Jackson, bingwa wa mbio za mita 200, alikimbia kwa sekunde 10.72 kama mjamaica mwenza na bingwa mara tano Fraser-Pryce akiandikisha muda wa sekunde 10.77

Richardson aligonga vichwa habari za michezo mnamo mwaka wa 2021 baada ya vipimo vyake kuonesha kuwa alikuwa ametumia bangi na akazuiliwa kushiriki michezo ya Olimpiki huko Tokyo Japan.

Sadfa ni kuwa bi Richardson alifuzu kwa fainali hizo “kujaza idadi” au kama (fastest looser) baada ya kumaliza watatu katika mbio za kufuzu kwa fainali.

Haijalishi umeshindwa mara ngapi au umeanguka mara ngapi,
Inuka,Pangusa vumbi,
Jaribu tena… ipo siku utafaulu

 

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.