Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Yanga inahitaji sare yoyote au ushindi kufuzu hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wakishindana na Wasudan(El Merreikh)

Yanga inahitaji sare yoyote au ushindi kufuzu hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wakishindana na Wasudan(El Merreikh).

El Merreikh ya Sudan imetangulia hatua ya kwanza ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimishwa suluhu nyumbani dhidi ya Otoho d’oyo ya Congo Brazzaville.

El Merreikh imefuzu kwenda hatua ya kwanza ya mtoano kwa faida ya bao la ugenini baada ya leo kulazimishwa suluhu hiyo ya bila kufungana ambapo awali wiki moja iliyopita timu hizo zilifungana bao 1-1 ugenini nchini Brazzaville.

Yanga ambayo ilishinda kirahisi dhidi ya ASAS ya Djibouti kwa mabao 2-0 kesho watarudiana pale pale Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam Mabingwa hao wa Tanzania wakisomeka wakiwa nyumbani.

Yanga inahitaji sare yoyote au ushindi kufuzu hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa watakapokwenda kukutana na Wasudan hao.

Endapo Yanga itashinda moja kwa moja itaanzia ugenini nchini Rwanda ambako El Merreikh wamechagua Uwanja wa Huye kuwa Uwanja wao wa nyumbani.

Timu hizo zitarudiana wiki moja baadaye hapa nchini kuamua timu ipi itinge hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.