Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA Crimean-Congo haemorrhagic fever (CCHF),CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

Crimean-Congo haemorrhagic fever (CCHF) ni ugonjwa ambao unaweza kuenea kwa kasi sana na ugonjwa huu husababishwa na virusi wanaojulikana kama tick-borne virus (Nairovirus) ambao wapo kwenye kundi la Bunyaviridae.

Virusi hawa huweza kusababisha mtu kuwa na homa kali ambayo huambatana na damu kutoka,kuisha pamoja na vifo kwa watu mbali mbali.

Tatizo hili la CCHF hutokea sana maeneo ya bara la Africa,Congo,Mashariki ya kati pamoja na nchi mbali mbali za Asia na virusi wake hupatikana kwa wanyama kama mbuzi,kondoo,ng’ombe,ndege pamoja na viroboto au ticks, hivo watu ambao hujihusisha na mifugo kama wafugaji wapo kwenye hatari zaidi ya kupatwa na ugonjwa huu

Binadamu hupata maambukizi ya virusi hawa kutoka kwa wanyama endapo amegusa damu au tisu za wanyama wenye virusi hawa baada ya kuchinjwa, na Maambukizi yake huweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine endapo mtu kagusa damu,mate,maji maji au jasho kutoka kwa mgonjwa mwenye ugonjwa huu.

DALILI ZA UGONJWA HUU WA Crimean-Congo haemorrhagic fever (CCHF) NI PAMOJA NA;

– Joto la mwili kupanda sana au mtu kuwa na homa kali kwa gafla

– Mwili kuchoka sana pamoja na misuli ya mwili kukosa nguvu kabsa

– Mtu kupatwa na hali ya kizunguzungu kikali

– Mtu kupatwa na maumivu makali ya shingo pamoja na shingo kukakamaa

– Mtu kupatwa na maumivu makali ya mgongo

– Mtu kupata maumivu makali ya kichwa cha mara kwa mara

– Mtu kupata vidonda kwenye macho,macho kuwasha pamoja na kukimbia mwanga

– Dalili zingine ni kama vile;

Mtu kuhisi kichefuchefu na kutapika,

Mtu kuharisha sana,

Mtu kupata maumivu makali ya tumbo,

Mtu kupata maumivu wakati wa kumeza kitu kooni

Kuvimba kwa lymph nodes

Mapigo ya moyo kwenda mbio sana n.k

VIPIMO VYA TATIZO HILI

vipo vipimo mbali mbali ambavyo huweza kufanyika maabara ili kugungua maambukizi ya virusi hawa kwa mtu,kama vile;

– enzyme-linked immunosorbent assay (ELISA) ;

– antigen detection;

– serum neutralization;

– reverse transcriptase polymerase chain reaction (RT-PCR) assay; and

– virus isolation by cell culture n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI LA CCHF

Ugonjwa huu huweza kuhusisha Matumizi ya dawa mbali mbali jamii ya antiviral drug kama vile; ribavirin pamoja na dawa zingine ambazo hutumika kudhibiti dalili zote ambazo hutokana na ugonjwa huu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.