Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

AINA ZA BIMA YA AFYA ZINAZOPATIKANA NCHINI TANZANIA

AINA ZA BIMA YA AFYA ZINAZOPATIKANA NCHINI TANZANIA

1. National Health Insurance Fund (NHIF)

2. Social Health Insurance Benefit (SHIB)

3. Community Health Fund (CHF) 

4. Tiba Kwa Kadi (TIKA)

5. Pamoja na Bima zingine zote za afya za makampuni binafsi ambazo ni Private health insurance Companies

NB: Kutokana na Takwimu za Mwaka 2019 kuhusu Health insurance coverage nchini Tanzania zinaonyesha kwamba; asilimia 32% ya Watanzania ndyo Wanaotumia Bima ya afya ambapo;

• Asilimia 8%- Ni wanachama wa Bima ya Taifa yaani  National Health Insurance Fund (NHIF)

• Asilimia 23%- Ni wanachama wa Community Health Fund(CHF)
• Asilimia 1%- Ni wanachama wa Bima za afya za makampuni binafsi yaani Private health insurances Companies

1. National Health Insurance Fund (NHIF)

Bima hii ya Afya ya Taifa imeanzishwa chini ya sheria ya Bunge “the Act of Parliament No. 8 ya mwaka 1999 ” na kisha kuanza kufanya kazi kuanzia June 2001,

Mwanzoni bima hii ililenga zaidi watumishi wa uma yaani Public Servants lakini kwa hivi sasa hata ambao sio watumishi wa Uma wanaweza kutumia Bima hii ya Afya.

2. Social Health Insurance Benefit (SHIB)

Bima hii ya afya ni sehemu ya National Social Security Benefits iliyoanzishwa mwaka 2007,ambapo wanachama wote wa mfuko wa NSSF walikuwa wanapata huduma za afya kupitia Bima hii.

3. Community Health Fund (CHF) na Tiba Kwa Kadi (TIKA)

Community Health Fund (CHF)-Hii ni Bima ya afya ambayo ililenga sana jamii nzima kwa ujumla ambayo ipo maeneo ya kijijini pamoja na watu wachini kabsa na kujiunga kwenye bima hii ni Hiari yako mwenyewe,tofauti na bima zingine za afya kama ya taifa NHIF ambapo ilikuwa nilazima mtumishi wa uma kukatiwa Bima hii ya Afya.

Tiba Kwa Kadi (TIKA),hii ilikuwa tofauti kidogo na Community Health Fund (CHF), kwani ililenga zaidi jamii ambazo zipo maeneo ya Mjini

– Kwa pamoja CHF na TIKA ziliundwa chini ya CHF act 2001 na kufanya kazi kwenye maeneo ngazi ya Wilaya. Ambapo kwenye ngazi hiyo ya Wilaya, council health service boards (CHSB) na health facilities governing committees (HFGC) ndyo wahusika wakuu wa kusimamia utendaji kazi wa CHF, Lakini mnamo mwaka 2009 Kazi zote za CHF kitaifa zilikabidhiwa kwa NHIF.

4. Bima zingine zote za afya za makampuni binafsi ambazo ni Private health insurance Companies

Hapa ni bima za makampuni yote binafsi yawe ni ndani ya Tanzania au Nje ya nchi wana Bima zao za afya, hapa huweza kuhusisha kampuni au hata mtu Binafsi pia

Mpango huu ulianzishwa miaka ya (2002) ambapo kulikuwa na Bima za afya binafsi yaani private health insurance firms in Tanzania, na ndipo mpango ukawa mkubwa zaidi hadi kuhusisha makampuni mbali mbali pia kama vile AAR, Jubilee Insurance, Resolution Health and Metropolitan Insurance.

Source:Wikipedia

KWA MAELEKEZO ZAIDI,INGIA KWENYE WEBSITE YA KILA AINA YA BIMA UNAYOTAKA, HUKO UTAPATA MAELEKEZO YAKE KAMILI ikiwemo jinsi ya kuwasiliana nao, NA JINSI YA KUPATA BIMA YAKO.

 

 

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.