Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Bungeni Dodoma,SPIKA Tulia: kuhusu bandari bunge limemaliza mjadala

Bungeni Dodoma,SPIKA Tulia: kuhusu bandari bunge limemaliza mjadala:

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amesema Bunge lina mipaka katika kujadili suala la uwekezaji wa bandari na liliishamaliza mjadala huo, hivyo wanachotakiwa kufanya hivi sasa Wabunge ni kuendelea kuwasikiliza Wananchi.

Dkt. Tulia ameweka wazi kuwa Bunge linawakilisha Wananchi na kuishauri Serikali, hivyo kama litaletewa mkataba wa bandari kwa utaratibu mwingine wa kibunge itakuwa ruksa kwa Wabunge kuchangia.

“Waheshimiwa Wabunge tulienda majimboni tumewasikia Wananchi, lakini pia tumewasikia wale wasio wa majimbo yetu wakiendelea kutoa maoni ya mambo mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. Uwekezaji bandari sisi kama Wabunge ni kazi yetu kuendelea kuwasikiliza Wananchi na kuisimamia Serikali.” amesema Dkt. Tulia

Spika Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma leo Agosti 29,2023 mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

#Bungeni
#Tanzania

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.