Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Zaidi ya watu 40 wahofiwa kufariki Mashariki mwa Kongo

Zaidi ya watu 40 wahofiwa kufariki Mashariki mwa Kongo

Idadi ya watu waliofariki kutokana na msako wa jeshi uliofanywa siku ya Jumatano dhidi ya waandamanaji wanaoupinga Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kigeni Mashariki mwa Kongo, imefikia takriban watu 40

Wanajeshi wa kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Bunagana

Jeshi la Kongo lilitawanya kwa nguvu maandamano hayo mjini Goma baada ya kanda ya video iliyoonesha shambulizi dhidi ya afisa wa polisi kusambazwa katika mitandao ya kijamii. Hata hivyo kanda hiyo haikuweza kuthibitishwa. Mamlaka inasema kuwa afisa huyo aliuawa kwa kupigwa mawe na kwamba waandamanaji sita waliuawa jeshi lilipoingilia.

Hospitali zimekuwa zikipokea malori yaliobeba maiti

Lakini maafisa hao wawili wa jeshi waliozungumza kwa sharti la kutotambulishwa, wamesema hospitali zimekuwa zikipokea malori kadhaa yaliobeba maiti tangu maandamano hayo kuanza na kusema idadi hiyo ni zaidi ya watu 40.

Chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa, kimesema wanachunguza madai ya vifo zaidi ya hamsini baada ya wanajeshi hao kuwazuia waandamanaji waliokuwa wamekusanyika kanisani kabla ya kuanza kwa maandamano hayo.

Hata hivyo msemaji wa jeshi la Kongo Luteni Kanali Guillaume Ndjike amekanusha ripoti hiyo na kusema ni watu saba pekee waliopoteza maisha.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.