Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Huduma ya Posta yahusika Katika Ukombozi wa Afrika

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Posta ilikuwa na mchango mkubwa katika ukombozi wa bara la Afrika dhidi ya ukoloni kwa kuwa hitaji kubwa kwa nyakati hizo lilikuwa ni kutumiana barua na taarifa kwa njia ya posta.

Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo la makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya mawasiliano.

Sambamba na hilo, Rais Samia amebainisha kuwa Umoja wa Posta Afrika unaweza kuleta mageuzi makubwa kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya bara la Afrika.

Amesema hayo yanawezekana kwa sababu Posta ilichangia kuleta uhuru Afrika kwa nyakati hizo, hivyo hivi sasa inaweza kuleta mabadiliko ya kidigitali katika huduma za posta ndani ya Afrika.

 

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.