Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DAWA AMBAZO HAZIRUHUSIWI KUTUMIA NA POMBE

Kwanza kabla ya kuangalia dawa ambazo haziruhusiwi kuchanganya na pombe,tuangalie nini kinatokea endapo mtu akinywa dawa pamoja na pombe,soma hapa chini;

– Pombe huweza kuifanya dawa ambayo umekunywa isifanye kazi vizuri kama inavyotakiwa(less effective)

– Kwa maana nyingine pombe huweza kupunguza uwezo wa dawa kufanya kazi

– Pombe huweza kuifanya dawa uliyokunywa kuwa sumu mwilini badala ya kuwa tiba

– Pombe huweza kuongeza maudhi ya dawa(side effects) kwenye mwili wako

– Pombe huweza kusababisha mtu kupata dalili mpya baada ya kunywa dawa ambazo mwanzoni hakuwa nazo au kupelekea ugonjwa kuzidi mwilini

DAWA AMBAZO HAZIRUHUSIWI KUTUMIA NA POMBE NI PAMOJA NA;

1. Dawa za maumivu jamii ya Ibuprofen,asprin na acetaminophen,

Matumizi ya pombe pamoja na ibuprofen(Motrin,naproxin) huweza kusababisha mvurugiko wa tumbo,tumbo kuwa na vidonda pamoja na kuvuja damu

Acetaminophen pamoja na pombe vyote huvunjwa vunjwa na Ini, hivo matumizi ya vyote kwa pamoja husababisha Ini lako liwe buzy zaidi na kuvunja vunja pombe hivo kuacha dawa kama acetaminpohen kujikunsanya mwilini na kusababisha tatizo la Ini kuharibiwa yaani serious liver damage

2. Matumizi ya dawa jamii ya anti-anxiety pamoja na dawa za usingizi haziruhusiwi kuchanganya na pombe, dawa hizo ni kama vile;

– Lorazepam

– Alprazolam

– Diazepam

– Clonazepam n.k

3. Matumizi ya dawa jamii ya antidepressants na mood stabilizers,dawa hizo ni kama vile;

Aripiprazole,divalproex,lithium n.k, kuchanganya dawa hizi na pombe huweza kusababisha madhara mbali mbali kama vile;

– mtu kupata kizunguzungu kikali

– Kuongeza tatizo la depression

– mtu kushindwa kutembea

– Matatizo kwenye moyo n.k

4. Matumizi ya dawa jamii ya ADHD medications kama vile,Amphetamine,methylphenidate,lisdexamfetamine n.k

5. Matumizi ya dawa jamii ya antibiotics kama vile,Metronidazole maarufu kama Flagyl huweza kusababisha madhara kama vile mtu kuhisi kichefuchefu kikali pamoja na kutapika,

dawa zingine ni pamoja na; Nitrofurantoin,Isoniazid,Azithromycin n.k

6. Matumizi ya dawa jamii ya Nitrates pamoja na dawa zingine za Presha,ukichanganya dawa hizi pamoja na pombe mtu huweza kupata madhara mbali mbali kama vile;

– kizunguzungu kikali

– Mtu kuzimia kabsa

– Mapigo ya moyo kwenda mbio sana

– Au Mapigo ya moyo kubadilika kabsa yaani arrhythmias

7. Matumizi ya dawa mbali mbali za ugonjwa wa sukari,dawa hizo ni kama vile; Metformin,glyburide,Glipizide(Glucotrol) n.k

Kuchanganya dawa hizi pamoja na pombe huweza kusababisha kiwango cha sukari kwenye damu kuzidi kuwa chini badala ya kuongezeka,mtu kuhisi kichefuchefu na kutapika,maumivu makali ya kichwa,mapigo ya moyo kwenda mbio,mabadiliko ya gafla ya presha au shinikizo la damu

8. Matumizi ya dawa jamii ya warfarin au Coumadin,tumia dawa hizi kwa maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya pamoja na uangalizi wa karibu sana

9. Matumizi ya dawa za mafua na kikohozi kama vile; Pseudoephedrine,Guaifenesin,Oseltamivir n.k

10. Matumizi ya dawa kwa wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume,uume kutokusimama au Erectile dyfunction medications kama vile; Tadalafil,Sildenafil(Viagra),Vardenafil n.k

Dawa hizi ukichanganya na pombe huweza kuleta madhara mbali mbali kama vile;

– Mtu kupata tatizo la presha kuwa chini yaani low blood pressure

– Mtu kupatwa na hali ya kizunguzungu kikali

– Mtu kupata maumivu makali ya kichwa

– Pia pombe yenyewe huweza kusababisha tatizo la uume kushindwa kusimama pamoja na matatizo mengine mengi kwenye mfumo wa uzazi

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.