Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Zaidi ya watu 800 wamefariki dunia baada ya tetemeko la ardhi nchini Morocco

Zaidi ya watu 800 wamefariki dunia baada ya tetemeko la ardhi nchini Morocco:

Zaidi ya watu 800 wamefariki dunia baada ya tetemeko la ardhi kutokea nchini Morocco Ijumaa usiku.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imesema watu wengine zaidi ya 600 wamejeruhiwa katika janga hilo.

Tetemeko hilo kubwa lisilo la kawaida limesababisha uharibifu wa majengo katika vijiji vya milima ya Atlas hadi kwenye mji wa kihistoria, #Marrakech.

Wengi wa waliokufa ni kutoka katika mikoa mitano iliyo karibu na eneo lililoathiriwa zaidi na tetemeko hilo.

Idadi ya vifo na majeruhi inatarajiwa kuongezeka wakati waokoaji wakifukua vifusi vya majengo yaliyoanguka na wakijaribu kuyafikia maeneo yasiyofikika kwa urahisi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.