Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Huduma Bora za Afya Kuimarishwa ili Kupunguza vifo Vitokanavyo na Uzazi

JUHUDI za kuendelea kuhakikisha hakuna vifo Vitokanavyo na uzazi Kwa mama na mtoto wakati wa kujifungua,limepewa kipaumbele katika Utekelezaji wa afua mbalimbali za afya hapa nchini.

Katika kufanikisha mpango huu ,Wizara ya afya Kupitia idara ya afya ya uzazi mama na mtoto KwA kushirikiana na Ofisi Ya Rais TAMISEMI, inaendelea kuwakutanisha wadau wa maendeleo pamoja na viongozi wa mikoa na halimashauri kupitia vikao maalumu vya Kanda vinavyofanyika katika mikoa 9 ikiwemo ,Ruvuma,Iringa ,Njombe,Simiyu ,Mara ,Mwanza,Shinyanga ,Kagera na Geita

Baada ya kukamilisha kikao kilichofanyika Kanda ya ziwa Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI,Idara ya Afya ,Ustawi wa Jamii na Lishe kitengo Cha mama na Mtoto Marry Shadrack, amesema kuwa ,Suaa la dawa na Vifaa tiba ,vinavyomsaidia mtoto ni miongoni mwa mikakati inayotarajiwa kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa na kibobezi,hali kadhalika kuongeza upatikanaji wa dawa katika maeneo yote ya kutolea huduma.

“KwA kupata taarifa sahihi na kwa wakati sahihi kutoka eneo Husika hii itawezeha kuelekeza matumizi ya kifedha Ili kukidhi uhitaji kwa wakati huo,”alisema Marry.

Washiriki kutokea Kanda ya ziwa waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Waaganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri,Wakurugenzi wa Halmashauri,Wauguzi wakuu wa mikoa na halimashauri.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.