Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Simone Biles: Mwanariadha aliyepambwa kwa medali zaidi duniani katika mashindano ya sarakasi

Simone Biles: Mwanariadha aliyepambwa kwa medali zaidi duniani katika mashindano ya sarakasi

ReutersCopyright: Reuters

Biles alichukua dhahabu kwa alama 58.399

Mmarekani Simone Biles amekuwa mwanariadha aliyepambwa zaidi katika historia baada ya kushinda medali yake ya pili ya dhahabu katika Mashindano ya Ulimwengu ya Sarakasi.

Baada ya kuisaidia Marekani kutwaa taji la saba mfululizo la timu mapema wiki hii, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alishinda dhahabu ya pande zote nchini Ubelgiji siku ya Ijumaa.

Amepata jumla ya medali 34 za dunia na Olimpiki ni nyingi kuliko mwanariadha mwingine yeyote, wa kiume au wa kike.

Biles alichukua dhahabu kwa alama 58.399.

Alimaliza mbele ya bingwa mtetezi Rebeca Andrade wa Brazil (56.766), huku mwenzake wa Biles’ Mmarekani Shilese Jones akitwaa shaba kwa alama 56.332.

Ushindi huu ulikuwa taji lake la sita la dunia nzima hadi kufikia jumla ya medali 27 za dunia, ambazo ni pamoja na 21 za dhahabu.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.