Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Tanzania Na India yajadili Kuanzisha Kituo Cha Dawa Asilia

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan inafanya mazungumzo na Serikali ya India kuhusu kuanzisha kituo cha dawa asilia.

Hayo yamebainishwa kufuatia mazungumzo yaliyofanywa na ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Rais Samia kwa Serikali ya India kupitia Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi katika ziara ya Rais Samia nchini India.

“Mbali na kuwa tayari India inaisaidia Tanzania katika masuala ya ubobezi wa kupandikiza figo na uboho (bone marrow), pia viongozi hao wamejadili namna ya
kuanzisha kituo cha dawa asilia”imeandikwa kwenye taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi. Zuhura Yunus.

Rais Samia ameongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika ziara iliyolenga kukuza uhusiano wao wa kihistoria baina ya Tanzania na India kwa kiwango cha ushirika wa kimkakati.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.