Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Serikali kushirikiana na hospitali za max nchini india kuanzisha huduma ya upandikizaji wa ini

Serikali ya Tanzania imesaini hati ya makubaliano na Mtandao wa Hospitali za MAX nchini, India, makubaliano hayo yanalenga kuimarisha huduma za kibingwa na bobezi katika hospitali za rufaa nchini, kuwajengea uwezo kwa kutoa mafuzo ya muda mfupi na mrefu kwa wataalam wetu ili kufanikisha huduma mbalimbali za kibobezi ambazo kwa sasa hazipatikani hapa nchini.

Kupitia makubaliano hayo hospitali za Max kwa kushirikiana na Hospitali za hapa nchini zinatarajia kuanzisha huduma za matibabu ya upandikizaji wa Ini. Ikumbukwe kuwa, mnamo mwaka 2017 hospitali ya BLK-Max kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili walianzisha huduma za upandikizaji wa figo.

Aidha, kwa shirikiana na JKCI walianzisha huduma za matibabu ya kibingwa ya tiba za upasuaji mkubwa wa moyo.

Tunaamini ushirikiano na hospitali za Max utaboresha huduma za kibingwa na bobezi hapa nchini na kufanikisha ndoto ya Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuifanya Tanzania kuwa Kitovu cha Utalii Tiba katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Aidha, Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Hospitali za Max, Bwana Abhay Soi amemuakikishia Mhe. Rais Samia kuwa hospitali yake itaendelea kusaidia Serikali kuboresha upatikanaji wa huduma za kibingwa na bobezi nchini.

Bwana Soi amemueleza Mhe. Rais kuwa Hospitali yake iko tayari kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini kufanikisha ndoto ya Mhe. Rais ya kuigeuza Tanzania Kitovu cha Utalii Tiba.

Katika kutekeleza ahadi yake kwa Mhe. Rais, terehe 16 hadi 20 Novemba 2023 Madaktari Bingwa 9 kutoka katika hospitali ya BKL-Max, New Delhi watatembelea nchini kuja kufanya kambi za upasuaji wakishirikiana na Madaktari Bingwa katika hospitali za Taifa za Muhimbili, Mloganzila, MOI, JKCI, Hospitali ya Saratani ya Ocean Road na hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar (tarehe 20 Novemba 2023).

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.