Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Watu 500 wakiwemo Wagonjwa na Madaktari wanahofiwa kuuawa Gaza

Watu 500 wakiwemo Wagonjwa na Madaktari wanahofiwa kuuawa kwenye shambulizi ambalo limefanywa Hospitalini Ahli Arab katika Ukanda wa Gaza na tayari Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ametangaza siku tatu za maombelezo baada ya mashambulizi hayo.

Mtandao wa @DW_Kiswahili umeripoti kuwa Wizara ya Afya ya Hamas imedai shambulizi la angani la Israel lililofanywa usiku wa kuamkia leo ndilo limesababisha maafa hayo lakini Jeshi la Israel limekana kuhusika na kusema roketi ya Wanamgambo wa Kiislamu huko Gaza ndiyo imepiga Hospitali.

Kwa mujibu wa Israel, Intelijensia ya Jeshi lake imebaini kuwa roketi iliyofyatuliwa vibaya na Wanamgambo wa Gaza ndiyo imeshambulia Hospitali ya Ahli Arab.

Haya yanajiri wakati Rais wa Marekani Joe Biden akitarajiwa kuitembelea Israel leo Jumatano, siku moja baada ya ziara ya Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Tel Aviv.

Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amelaani shambulizi hilo na kutaka ulinzi wa haraka kwa raia na vituo vya afya katika eneo hilo la Palestina, Umoja wa Ulaya, Saudi Arabia, Jordan na Qatar ni miongoni mwa Nchi ambazo zimelaani shambulizi hilo zikisema zinakiuka sheria ya Kimataifa

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.