Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Watu wanne wamekufa leo Ijumaa katika mji wa Kericho, magharibi mwa Kenya

Watu wanne wamekufa leo Ijumaa katika mji wa Kericho, magharibi mwa Kenya, kufuatia mkanyagano uliotokea baada ya kuzuka hofu miongoni mwa watu waliokuwa wakisubiri kuingia uwanjani kusherehekea siku ya kitaifa ya mashujaa.

Polisi wamesema umati wa watu ulianza kutawanyika baada ya kuona moshi uliotokana na chai iliyomwagika na kudhani ilikuwa mabomu ya machozi.

Taarifa kutoka kituo cha Polisi cha Kericho imesema waliofariki wote ni wanawake, na watu wengine 13 wamejeruhiwa na kuwahishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kericho.

Na nchini Tanzania, Michuano mipya ya soka inayofahamika kama African football League inazinduliwa rasmi leo nchini Tanzania kwa mchezo wa kukata na shoka baina ya wenyeji Simba inayowakaribisha Al Ahly ya Misri.

Hii ni mara ya kwanza ligi hiyo kuanzishwa barani humu ikijumuisha timu nane. Wageni mbalimbali wanatarajia kuhudhuria uzinduzi huo, akiwamo rais wa shirikisho la soka duniani #FIFA, Gianni Infantino.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.