Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la Mzio na maji,chanzo,dalili na Tiba yake(Aquagenic Urticaria)

Aquagenic Urticaria maana yake ni pale ambapo mtu ana mzio(allergy) na maji, tunafahamu kwamba unaweza kupata allergic reactions kwa vitu mbali mbali ikiwemo;

  • Baadhi ya vyakula
  • Mafuta ya kupikia
  • Mafuta ya kupaka
  • Sabuni za kuogea
  • Perfumes mbali mbali n.k

Ila kwa mtu mwenye tatizo la Aquagenic urticaria huwa ana mzio au allergy na maji.

Tatizo hili ni adimu sana kutokea ila lipo, na watu wenye tatizo hili hupata shida sana baada ya kugusa au kutumia maji,

Dalili za Ugonjwa huu wa Mzio na maji

Moja ya dalili kama una mzio au allergy na maji ni pale ambapo baada ya kugusa au kutumia maji unapata matokeo kama haya, Ndani ya dakika chache watu walio na hali hii wanaweza:

– Kupata upele kwenye Ngozi, na mara nyingi upele huu huonekana kwenye maeneo kama vile; Kifuani,Shingoni, kwenye mikono n.k

Wakati mwingine inaweza kuonekana mahali popote kwenye mwili isipokuwa kwenye nyayo za miguu na viganja vya mikono.

– shida ya ngozi kubadilika rangi na kuwa nyekundu zaidi(erythema)

– Kuhisi hali ya kuunguza au vitu vinachoma choma mwilini

– Mwili kuvimba baada ya kugusa au kutumia maji n.k

NB:Moja ya madhara ambayo huonekana kwao baada ya kugusa au kutumia maji ni pamoja na;

  • Kuwa na upele kwenye ngozi ya mwili
  • Kuhisi hali ya kuungua mwilini
  • Mwili kuvimba
  • Kuwa na vidonda mwilini
  • Ngozi ya mwili kuwa nyekundu sana
  • Ngozi kuwasha sana
  • Ngozi kupata mchubuko,
  • Ngozi kuwa na magamba au kutoka magamba n.k

Kama nilivyosema hapo awali Ndani ya dakika chache watu walio na hali hii ya Mzio na Maji wanaweza kupata hizi dalili baada ya kugusa au kutumia maji, na kama umetoka kuoga na ukakausha mwili wako, dalili zinapaswa kuanza kuisha ndani ya dakika 30 hadi saa 2.

Kwa baadhi ya Watu wenye tatizo hili la Mzio na maji, baada ya Kunywa maji huanza kupata matokeo kama haya;

  • Kuvimba Lips za mdomo
  • Kupata upele au rashes kuzunguka mdomo n.k

Lakini kwa Watu ambao tatizo hili linawasababishia madhara makubwa sana(severe cases), wanaweza kupata matatizo kama vile;

– Kupata shida ya kumeza kitu

– Kukosa pumzi au kupata shida ya kupumua

– Kutoa sauti wakati wa kupumua(wheezing) n.k

Wahi hospital mapema kama unapata dalili kama hizi.

Matibabu ya Tatizo hili la Mzio wa Maji

Kwa bahati mbaya mpaka sasa hakuna tiba kamili ya kuondoa kabsa tatizo hili, ila kuna matibabu ya kudhibiti dalili zinazotokana na tatizo hili.

Mfano; ukiwa na dalili kama vile; kupata muwasho sana kwenye ngozi,kuvimba n.k utapewa dawa jamii ya antihistamine,

Hivo hakikisha unapata msaada wa wataalam wa afya kama unapata shida kama hii.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.