Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Waziri Mkuu Atembelea shamba la Kisasa la Mifugo -Italia

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea shamba la ufugaji wa ng’ombe wa maziwa la Alesandra lililopo Milan nchini Italia, ambalo linaendeshwa kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kielektoniki ikiwemo ukamuaji wa maziwa kwa kutumia roboti.

Akiwa katika shamba hilo lenye takribani ng’ombe 500 Waziri Mkuu Majaliwa ameshuhudia mifumo bora ya ufugaji, ulishaji, unyonyeshaji na ukamuaji wa maziwa, ambapo ng’ombe mmoja ana uwezo wa kutoa lita kuanzia 35 hadi 70 kwa siku.

Waziri Mkuu ameeleza kufurahishwa na teknolojia inayotumika katika ufugaji huo.

Waziri Mkuu Majaliwa yupo nchini Italia akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.