Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Ocean Road,kwa siku watu 600 wanakuja na kuondoka na 100 wanalazwa

Wakati mapato ya kodi yanayotokana na michezo ya kubahatisha yanapaa kutoka Sh85 bilioni mwaka 2019/2020 hadi Sh168 bilioni mwaka 2022/2023, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT) imetoa msaada kwa wagonjwa na wafanyakazi katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.

GBT kwa kushirikiana na wadau imetoa msaada huo wenye thamani ya Sh40 ikiwa ni moja kati ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa kwake nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa GBT), James Mbalwe amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuigusa jamii na kuwatia moyo madaktari na watoa huduma za afya ili waendelee na kazi hiyo.

“Katika kuadhimisha miaka 20 ya kuanzisha kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) tumeona tuwaguse wagonjwa na kuwatia moyo madaktari na wahudumu kwa kuleta vifaa na mchango wa kifedha,”amesema Mbalwe.

“Sisi GBT pamoja na washirika wetu kadhaa tumetoa misaada yetu yenye jumla ya Sh40 milioni,”amesema na kuongeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk Julius Mwaiselage amesema msaada huo wa vifaa na fedha utawasaidia kwani idadi ya wagonjwa wa saratani inazidi kuongezeka nchini na mahitaji bado hayakidhi haja.

“Tunawapongeza GBT kwa kutoa msaada katika taasisi yetu, ni misaada ambayo tunaihitaji sana, vifaa hivi vitaenda kuwasaidia wagonjwa waliolazwa na wale wanaoenda na kurudi,”amesema.

Dk Mwaiselage amesema watu 100 hulazwa hospitalini hapo ambao kwa wastani hukaa zaidi ya wiki tatu, hivyo mahitaji ni makubwa nab ado wanahitaji misaada mingi zaidi.

‘Ugonjwa wa Saratani unaongezeka nchini kwa siku watu 600 wanakuja na kuondoka na 100 wanalazwa hapa hivyo mahitaji ni mengi,”ameongeza.

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ni chombo cha udhibiti wa michezo ya bahati nasibu ambacho kilianzishwa chini ya Sheria ya Michezo ya Kubahatisha na kuanza kutumika Julai 1, 2003 huku ikiwa na jukumu la kusimamia, kufuatilia na kudhibiti uendeshaji wa shughuli za michezo ya kubahatisha nchini Tanzania.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.