Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio waafrika tu peke yake hata wazungu wengi husumbuliwa na shida hii ya mgongo kuwaka moto, soma hapa chini;

Kutokana na takwimu za Taasisi ya “National institute of Neurological disorders and strokes” huko marekani inasema kwamba,Asilimia 80% ya Wamarekani husumbuliwa na shida hii ya mgongo kuwaka moto kwenye vipindi flani tofauti vya maisha kwa kila mtu,

Je shida hii ya mgongo kuwaka moto chanzo chake ni nini?, Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kusababisha mtu kupata shida hii ya mgongo kuwaka moto,

CHANZO CHA TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO NI PAMOJA NA;

1. Mtu kufanya kazi ambazo zinahusu kukaa kwenye vyanzo vya moto kwa muda mrefu,kama vile kazi za kupika,kuchomelea,au mtu kuchomwa na jua sana au kuunguzwa na moto

2. Ugonjwa unaotokea kwenye pingili za uti wa mgongo maarufu kama Degenerative Disc disease, kutokana na sababu mbali mbali kama vile: pingili kusagika, pingili za uti wa mgongo kuzeeka(aging) n.k

3. Shida ya Misuli kukaza kuliko kawaida yaani Muscle strains

4. Shida ya nerves eneo la uti wa mgongo kubanwa zaidi yaani Spinal cord nerves compression

5.Mtu kupata majeraha yoyote au kuumia kwenye uti wa mgongo

6. Mtu kupatwa na shida ya uvimbe unaotokea eneo la uti wa mgongo au spinal cord tumor

7. Uharibifu wa Mfumo wa Nerves kutokana na matumizi ya pombe kupita kiasi,tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Alcohol Neuropathy

8. Uharibifu wa Mfumo wa Nerves kutokana na ugonjwa wa Kisukari,tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Diabetic Neuropathy

9. Mtu kuwa na tatizo la upungufu wa vitaminis(Vitamin deficiency) ambapo huleta shida kwenye mgongo ikiwemo kwenye nerves pamoja na shida hii ya mgongo kuwaka moto

10. Mtu kupata shida ya mgongo kuwaka moto kutokana na mfupa wowote eneo la mgongoni kuvunjika

11. Uwepo wa Maambukizi kuzunguka eneo la uti wa mgongo nakusababisha shida kama vile Epidural abscess

12. Kuvimba kwa ubongo kutokana na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Virusi, hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Encephalitis,au mtu kupatwa na mashambulizi ya herpes Zoster n.k

13. Uwepo wa magonjwa ambayo huathiri ubongo pamoja na uti wa mgongo kama vile Multiple Sclerosis n.k

14. Uwepo wa tatizo la Rheumatoid arthritis,ambapo huhusisha mashambulizi ya kinga yako ya mwili mwenyewe yaani Autoimmune disease na kusababisha matatizo kama vile joint kuvimba,mgongo kuwaka moto n.k

15. Shida ya mwili kuzishambulia seli pamoja na Tisu na kusababisha matatizo kama vile Systemic Lupus Erytheimatosus disorder

16. Tatizo la kwenye nerves ambalo huhusisha kuvimba kwa uti wa mgongo,shida hii kwa kitaalam hujulikana kama Transverse Myelitis(Neurological disorder)

MATIBABU YA TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO

Kama nlivyokwisha kuelezea baadhi ya sababu za tatizo hili la mgongo kuwaka moto,Na matibabu yake hutegemea na chanzo husika, hivo kwa ujumla wake, Mfano;

kama mgonjwa anapata shida ya mgongo kuwaka moto kutokana na upungufu wa Vitamins(Vitamin deficiency) ambazo hupelekea shida kwenye nerves za uti wa mgongo,

Basi shida hii huweza kuhusisha matibabu ya matumizi ya dawa jamii ya Neuroton pamoja na Dawa zingine ambazo zitasaidia shida hii n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.