Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA KIFAFA(Epilepsy),CHANZO,DALILI NA TIBA

UGONJWA WA KIFAFA(Epilepsy),CHANZO,DALILI NA TIBA

Ugonjwa wa kifafa ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Epilepsy,ugonjwa huu huathiri mfumo mkuu wa fahamu yaani central nervous system (neurological disorder) ambapo husababisha shuhuli zote zinazofanywa na ubongo kufanyika isivyokawaida,

kisha kusababisha madhara mbali mbali kama vile mwili kutetemeka sana(seizures),mtu kuanza kufanya vitu vya ajabu(unusual behavior),mtu kudondoka chini gafla na wakati mwingine mtu kupoteza kabsa fahamu.

Mtu yoyote huweza kupata ugonjwa wa kifafa tofauti na watu wengi wnavyofikiria kwamba lazima uzaliwe na shida hyo,ugonjwa wa kifafa huweza kutokea hata kama hapo mwanzoni haukuwa nao, na hauchagui jinsia,umri wala kabila,

Kwa Mujibu wa Shirika la afya Duniani(WHO),

Ugonjwa wa Kifafa Umewapata Watu zaidi ya Million 50 Duniani kote

Huku Zaidi ya Asilimia 75% ya watu wanaoishi na Kifafa kwenye nchi za Kipato cha Chini hawapati Matibabu wanayohitaji.

DALILI ZA UGONJWA WA KIFAFA NI PAMOJA NA;

– Mtu kupatwa na hali kama ya kuchanganyikiwa au kutojielewa ambapo hutokea kwa muda kisha kutulia yaani Temporary confusion

– Mtu kuanza kuona vitu vya ajabu ajabu yaani staring spell

– Mtu kupatwa na hali ya misuli ya mwili kukakamaa

– Mtu kudondoka chini kwa gafla

– Mtu kuanza kutoa mate mdomoni huku yakishuka yenyewe mpaka chini

– Mtu kupatwa na hali ya mikono,miguu pamoja na mwili kugara gara

– Mtu kupoteza fahamu au kutojielewa,hali ambayo hutokea kwa muda na kupotea

– Mtu kuingiwa na hali ya wasiwasi au hofu kubwa n.k

KUMBUKA:UKIONA DALILI HIZI HAPA CHINI HATA KAMA IMEGUNDULIKA UNA UGONJWA WA KIFAFA,NENDA HOSPITAL MAPEMA ZAIDI;

Kama unaishi na mgonjwa wa kifafa ukiona kuna dalili hizi hapa chini mpeleke hospital mapema mgonjwa wako kwa ajili ya matibabu zaidi,

  • Hali ya mwili kutetemeka(seizure) ambayo hukaa kwa zaidi ya dakika Tano
  •  Hali ya kupoteza fahamu ambayo huendelea kuwepo hata kama mwili umeacha kutetemeka
  • Mgonjwa kuwa na homa kali au joto la mwili kuwa juu sana
  • Kupatwa na dalili zote za kifafa alafu wewe ni mjamzito
  • Kupatwa na dalili zote za kifafa alafu una ugonjwa wa Kisukari
  •  Umepatwa na majeraha kwa kuungua na moto n.k au kwa kujiumiza mwenyewe,nenda hospital kwa ajili ya matibabu
  • Kama ulikuwa na ugonjwa wa kifafa lakini ulikuwa hupati shida ya mwili kutetemeka yaani Seizure na sasa hyo hali ndyo imeanza

CHANZO CHA UGONJWA WA KIFAFA NI NINI?

Watu wengi wenye ugonjwa wa kifafa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo inajulikana kama chanzo chake,ila kutokana na tafiti mbali mbali sababu hizi hapa chini zimeonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa tatizo hili,na sababu hizo ni kama vile;

1.Sababu kwenye Vinasaba(Genetic influence). Hapa tunazungumzia swala la mtu kurithi vinasaba vya tatizo hili au Genes kutoka kwenye Familia yake au ukoo wake,
Hivo endapo shida hii ya kifafa ipo kwenye ukoo wenu au Familia yenu,uwezekano wa mtu yoyote kuzaliwa na shida hii ya kifafa ni mkubwa

2. Mtu kupata ajali yoyote ambayo inahusisha kugonjwa kichwani yaani Head trauma,mfano ajali ya Gari,piki piki n.k huweza kuchangia mtu kupatwa na tatizo la kifafa

3. Mtu kupatwa na matatizo mbali mbali kwenye ubongo wake(Brain abnormalities),Kama vile kupata uvimbe kwenye ubongo(brain tumors),matatizo kwenye mishipa ya damu ndani ya ubongo kama vile tatizo la arteriovenous malformations na cavernous malformations n.k.

4. Mtu kupatwa na tatizo la kiharusi au Stroke,Shida hii ya stroke ni kisababishi mojawapo kikubwa cha ugonjwa wa kifafa kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 35.

5. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile; Meningitis, HIV, viral encephalitis n.k huweza kuchangia mtu kuwa na tatizo la kifafa

6. Mtoto kupatwa na majeraha au kuumizwa kabla ya kuzaliwa yaani Prenatal injury, tatizo hili huhusisha sana ubongo wa mtoto kuumizwa au kuharibiwa kabla ya kuzaliwa kutokana na sababu mbali mbali kama vile;

mama kupatwa na mambukizi ya magonjwa mbali mbali wakati wa ujauzito mfano kaswende(syphilis),Lishe duni wakati wa ujauzito,mtoto kukosa hewa ya kutosha akiwa tumboni(oxygen deficiencies),Vyote hivi huweza kupelekea shida kwenye ubongo na matokeo yake ni mtoto kupatwa na tatizo la kifafa(epilepsy au cerebral palsy).

7. Mtoto kuzaliwa na kupatwa na matatizo mbali mbali katika ukuaji wake(Developmental disorders). Mfano mtoto kupatwa na tatizo la Usonji au autism huweza pia kusababisha tatizo hili la kifafa

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATWA NA UGONJWA WA KIFAFA NI PAMOJA NA;

1.Umri; Watoto wadogo pamoja na watu wenye umri mkubwa

2. Kuwa kwenye Familia ambayo inahistoria ya watu kuumwa kifafa

3. Waliopata ajali ambazo huhusisha mtu kugonjwa sana maeneo ya kichwani(Head injuries),mfano kutokana na ajali za Gari,Piki piki n.k

4.Wenye tatizo la Stroke pamoja na magonjwa mengine ambayo huhusisha mishipa ya damu yaani vascular diseases.

5. Wanaokunywa pombe kupita kiasi pamoja na wanaovuta sigara

6. Watu wenye ugonjwa wa Dementia. Ugonjwa huu huongeza uwezekano wa mtu kupata kifafa kwa Watu wenye umri mkubwa(Wazee)

7. Watu wenye Maambukizi ya magonjwa kwenye ubongo kama vile meningitis n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.