Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

“Kuna sindano nilikuwa nachoma sindano moja ni milioni 5” Prof. Jay

Mbunge wa zamani wa Mikumi na Msanii Staa Joseph Haule maarufu Prof. Jay amesema ameamua kuanzisha Professor Jay Foundation ambayo itazinduliwa Nov 24,2023 Jijini Dar es salaam,

kwasababu amelazwa Hospitali ameona Watu wanapata tabu sana na gharama za matibabu ya figo ni kubwa na wengine wanapoteza maisha kwa kukosa pesa za matibabu hayo.

Akiongea kwenye Power Breakfast ya @cloudsfmtz leo November 06,2023, Prof. Jay amesema “Kuna sindano nilikuwa nachoma sindano moja ni milioni 5 na kwa siku nachoma sindano mbili , milioni 5 asubuhi, milioni tano jioni, ile sindano ndio imeaniamsha na kwa wiki nilikuwa nachoma siku tano, ni milioni 50”

“Hiyo ni sindano tu bado dialysis (kusafisha damu kwenye figo) ukiwa umeanzia Muhimbili ni laki 1 na elfu 80 lakini kwa Mgonjwa anayetoka nje ni laki 3 na nusu hiyo ni mara moja na unatakiwa ufanyiwe mara tatu mpaka mara nne kwa wiki kutokana na hali yako”

“Kwa kuanzia nimeanza na Professor Jay Foundation kwasababu nimeona Watu wanapata tabu sana na hizi hela nyingi sana wanazotumia na wote hawawezi kufikiwa na Rais na Watu wanataabika sana,

kwangu ilikuwa kawaida lakini kuna Watu figo zimefeli, nilikuwa nachomwa hivyo lakini figo zangu zilikuwa hazijafeli ni kwamba figo moja ilikuwa na mchanga na moja ilikuwa inasuasua ilikuwa na sumu nyingi”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.