Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Issa Juma, Kaka yake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azikwa Ruangwa

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameungana na Viongozi mbalimbali wa kitaifa na Watanzania kwa kutoa salamu za pole kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kufuatia kifo cha Kaka yake, marehemu Issa Juma, aliyezikwa leo.

Akiongea November 06, 2023 Wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi wakati akitoa salamu hizo kwa niaba ya Mawaziri, Dkt. Biteko amesema Watanzania wanaupendo wa dhati kwa Waziri Mkuu Majaliwa ambao wameuonesha pia katika kipindi hichi cha kumpoteza marehemu Kaka yake.

“Sisi ni kielelezo kuwa Watanzania wana upendo nawe ndio maana tumekuja kuungana pamoja na wewe, kulia pamoja na wewe lakini kukutia moyo kwamba sisi tuliofika hapa na wengine tunakupa pole kwa msiba wa kumpoteza Kaka”

Amesema kuwa, jambo lolote linalotokea ni mipango ya Mwenyezi Mungu hivyo ni muhimu kuombeana heri ili tuwe na mwisho mwema duniani.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewashukuru Watanzania kwa kumfariji katika kipindi hichi cha msiba wa Kaka yake ambapo amesema amepokea salamu za pole kutoka kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Dkt.Hussein Mwinyi na Watanzania wote wanaompa pole na kumfariji.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.