Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Upandikizaji wa nyonga na magoti bandia watarajiwa kuanza – Mloganzila

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Hospitali ya Queen Elizabeth ya nchini Uingereza imesema inatarajia kufanya kambi maalumu ya upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia kwa wagonjwa wenye changamoto za maradhi ya nyonga na magoti kuanzia November 27,2023 hadi December 01,2023.

Daktari Bingwa wa Upasuaji Mifupa, Nyonga na Magoti, Dkt. Shilekirwa Makira amesema Wagonjwa watakaonufaika na huduma hizo ni pamoja na wenye matatizo ya nyonga zilizosagika zenye maumivu makali na magoti yaliyosagika ambapo watabadilishiwa kwa kuwekewa nyonga na magoti bandia kitu kitakachowafanya waondokane na maumivu wanayoyapata kabla ya nyonga zao kubadilishwa.

“Tungependa watu wajitokeze na kujisajili mapema kabla ya November 27,2023 ili Hospitali iweze kufanya maandalizi stahiki ikiwemo pamoja na kufanya vipimo vya awali ambayo ni muhimu kabla ya kufanya upasuaji huu”

Dkt. Makira amesema kwa waliojiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya, mfuko unagharimia zaidi ya asilimia 90, pia bima nyingine zinagharimia matibabu hivyo Watu wasisite kujitokeza kuchangamkia fursa hii adhimu.

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.