Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Madaktari wengine wanafanya upasuaji bila ganzi Gaza- WHO

Shirika la Afya Duniani linasema baadhi ya madaktari huko Gaza, Palestina wamekuwa wakifanya upasuaji, ikiwa ni pamoja na kukata viungo, bila ganzi.

Kufuatia shambulio la kikatili la wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7, 2023, na kuua watu 1400,  Israel imeanzisha mashambulizi makubwa Gaza huku takriban watu 10,000 wakiripotiwa kuuawa.

Operesheni ya kijeshi ya Israel, pia imesababisha kuzuiwa kwa Maji, chakula, mafuta na madawa muhimu katika eneo hilo dogo.

msemaji wa WHO Christian Lindmeier alisema Jumanne wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Geneva, akisisitiza “mahitaji yao makubwa ni maji, mafuta, chakula na upatikanaji salama wa huduma za afya ili kuishi.”

Kiwango cha vifo na mateso ni “vigumu kueleweka,” aliongeza.

Lindmeier pia alisema kuwa takriban wahudumu wa afya 16 wameuawa wakiwa kazini, akisisitiza kuwa mashambulizi yoyote dhidi ya huduma za afya yamekatazwa na sheria za kimataifa za kibinadamu.

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, pia linajulikana kama Médecins Sans Frontières, lilisema Jumanne kwamba mmoja wa wafanyakazi wenzake na baadhi ya wanafamilia wake waliuawa katika mlipuko katika kambi ya wakimbizi ya Al Shati.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.