Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Paul Makonda mpaka kwa Mama JPM,Bibi Suzana Magufuli

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda @baba_keagan akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Ziwa amefika kumsalimia Bibi Suzana Magufuli ambaye ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.

Itakumbukwa enzi za uhai wake wakati wa Kampeni Uchaguzi mwaka 2020, Hayati Magufuli aliwahi kuizungumzia hali ya afya ya Mama yake, September 09,2020 ambapo alinukuliwa akisema “Nakushukuru Mama Maria Nyerere kwa kuja kuniombea kura, una umri wa Mama yangu, wewe unatembea, Mama yangu yupo kitandani kwa zaidi ya miaka miwili anakula kwa kutumia mipira, siku tuliyokutana uliniambia Mama yako anaumwa kwa makusudi ya Mungu ili wengine tupone”

Baadaye October 10,2020 Hayati Magufuli akanukuliwa tena akisema “Kila mara namfikiria Mama yangu ambaye miaka miwili yupo kitandani hawezi kuongea anaumwa, ila alisimama kwa ajili ya Watoto wake, najua Wanawake wananyanyaswa kwenye mirathi n.k, ndio maana nimemchagua Mama Samia anisaidie kuwabeba Wanawake, Wanawake nitawabeba”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.