Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Watu wawili wamefariki mkoani Pwani mmoja kwa kusombwa na maji na mwingine kuzama wakati akiogelea

Matukio ya vifo hivyo yametokea kwa nyakati tofauti ikiwa ni sehemu ya madhara kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Jumanne Novemba 14,2023; Kamanda wa Polisi mkoa huo, Pius Lutuma amesema miongoni mwa waliofariki, ni pamoja na mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Chambasi, wilaya ya Kisarawe, ambaye kifo chake kimetokea wakati akiogelea jirani na makazi yao.

New Content Item (2)

“Huyu mwanafunzi alifariki baada ya kuzama dimbwi lililokuwa limejaa maji jirani na nyumbani kwao,” amesema kamanda huyo, huku akimtaja Ally Haji ambaye alifariki baada ya kusombwa na maji wakati wakati akijaribu kuvuka mto huko Mindukeni Chalinze mkoani Pwani.

“Alikuwa navuka kwenye mto uliopo maeneo ya Mindukeni lakini kwa bahati mbaya akasombwa na maji na mwili wake ukaokotwa na baadaye kupewa familia kwaajili ya shughuli za maziko,” amesema.

Kwa mujibu wa Kamnada hyo, matukio ya vifo hivyo yalitokea Novemba 13, 2023; ambapo ametoa tahadhari kwa wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari ya mvua kwa kipindi hiki ili kulinda usalama wao na mali zao.

Amesema kuwa jeshi hilo limeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuchukua tahadhari kipindi hiki mvua zinapoendelea kunyesha na kusisitiza kuwa wanapaswa kuzingatia hilo ili kulinda familia ikiwemo wanafunzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi mkoani Pwani wamesema kuwa wakati mvua zinaendelea kunyesha kuna umuhimu wa watu kutembea makundi makundi ili hata ikitokea bahati mbaya mmoja wao kutaka kusombwa na maji iwe rahisi kutoa msaada.

“Mvua zinaendelea kunyesha na kama mtu atatoka peke yake inakuwa ngumu kupata msaada pindi anapopatwa na shida hasa kusombwa na maji lakini mkiwa wengi inakuwa rahisi kusaidiana,” amesema Catherin John.

Kwa upande wake Sauda Shabani amesema kuwa wakati umefika ambao Serikali inapaswa kuweka utaratibu wa kutoa mafunzo ya ujuzi wa kuogelea kwa wakazi waishio mikoa inayopakana na mito ikiwemo Dar es Salaam na Pwani ili inapotokea wamekumbana na maji mengi iwe rahisi kukabiliana na hali hiyo.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.