Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Idadi ya vifo imefikia 80,Mafuriko Hanang

Serikali imetoa taarifa kuhusu maendeleo ya hali baada ya maafa ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na mawe kutoka mlima Hanang Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara, yaliyotokea alfajiri ya December 03, 2023 ambapo imesema hadi kufikia
saa 6:00 mchana leo December 08,2023 idadi ya vifo imefikia 80 (Watu wazima ni 48 wakiwemo Wanaume 19 na Wanawake 29) na Watoto ni 32 (wakiwemo wa kiume 15 na wa kike 17).

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali akiongea leo Katesh, Hanang, Manyara amesema “Mwili mmoja wa Mtoto wa kiume ambao ulikuwa haujatambuliwa hadi jana sasa umetambuliwa lakini kuna mwili wa Mwananke mmoja Mtu mzima uliopatikana leo ambao bado haujatambuliwa, hivyo jumla ya maiti zilizokwishatambuliwa hadi sasa ni 79”

“Kwa jumla hadi kufikia saa 6:00 mchana leo, idadi ya majeruhi waliopokelewa katika Hospitali zetu Mkoani Manyara ilifikia 133 (Watu wazima 71 na Watoto 62, kwa mujibu wa agizo la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waathirika wote wanatibiwa bure na pia serikali inagharamia mazishi ya waathirika wote”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.