Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

TAARIFA:Kuna Ongezeko la COVID na Mafua

Wizara ya Afya imesema imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa taarifa za magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na tetesi za kuwepo kwa magonjwa hayo ndani na nje ya Nchi ambapo kuanzia November, 2023,

kumekuwa na tetesi juu ya ongezeko la visa vya magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa sehemu mbalimbali duniani na ndani ya nchi hususan Dar es salaam ambapo imesema Covid 19 imeendelea kuwepo kwa kiwango cha chini kama magonjwa mengine ya mfumo wa njia ya hewa ukiongezeka na kupungua kwa nyakati tofauti za majira ya mwaka.

Wizara imesema virusi vya Influenza vilivyobainika nchini havina madhara makubwa ndio maana unaitwa ugonjwa wa majira (Seasonal Influenza) lakini hata hivyo takwimu za ufualitiliaji (surveilance) za Wizara zinaonesha ongezeko la maambukizi ya Covid 19 kutoka 37 mwezi October 2023 hadi maambukizi 65 mwezi December 2023”

“Aidha, ongezeko hili ni sambamba na ongezeko la maambukizi ya mafua yanayotokana na influenza kutoka maambukizi 34 hadi 49 katika kipindi hicho hicho”

“Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa na inaelekeza Wataalamu katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya kuendelea kufanya utambuzi kwa njia ya vipimo vya maabara na kutoa matibabu stahiki,

pia Wizara inashauri Wananchi kuwahi kwenye Vituo vya kutolea huduma mara wapatapo dalili za magoniwa ya mfumo wa njia ya hewa zikiwemo mafua, kikohozi, kuwashwa koo, kupumua kwa shida, homa na kuumwa kichwa” ——— imeeleza taarifa ya Wizara. Via:MillardAyoUPDATES

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.