Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Familia ya Mr. Ibu yakanusha ripoti kwamba mguu wake wa pili umekatwa

Familia ya mwigizaji anayeugua, John Okafor almaarufu Mr. Ibu imekanusha ripoti kwamba mguu wake wa pili umekatwa.

Mapema jana taarifa zilienea mitandaoni kuwa mguu wa pili wa mwigizaji huyo umekatwa.

Katika taarifa iliyotolewa jioni ya jana na kusainiwa na Valentine Okafor mmoja wa familia hiyo pia ilikanusha ripoti kwamba anapambana na ugonjwa wa Kisukari,

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwigizaji huyo mkongwe anapambana na tatizo la damu kuganda kwenye miguu yake. Ilielezwa kuwa hajasafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi kwa sababu madaktari wameeleza‘’Si salama kusafiri kwa ndege’’.

Taarifa hiyo inasomeka;

‘’Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Wanigeria na umma kwa ujumla kwa ajili ya michango yenu mikubwa, kimwili, kiroho na zaidi ya yote kifedha kwa kumrejesha baba yetu Bw John Okafor (Mr. Ibu) kwa miguu yake tena.

Tunataka kusahihisha baadhi ya dhana potofu zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hali ya sasa ya afya ya baba yetu.

Kwanza tungependa kusema kwamba baba yetu hakukatwa miguu yote miwili bali ni mmoja tu. Kukatwa kwa mara ya kwanza hakukusahihisha kabisa hali yake ya kiafya hivyo madaktari walilazimika kwenda mbele kumkata mguu huo huo ili kuhakikisha hatumpotezi.

Sababu ya ugonjwa wa baba pia si kisukari lakini amekuwa akipata tatizo la damu kuganda mara kwa mara kwenye mguu wake (mishipa iliyo na ugonjwa) na changamoto nyingine za kiafya zinazohatarisha maisha yake, kwa hivyo kupelekea uhitaji wa kukatwa.

Hatimaye, sababu pekee kwa nini familia haijamsafirisha nje ya nchi hadi sasa ni kwa sababu madaktari wamemuelezea kuwa “Hafai Kusafiri”..”Si salama kwake kusafiri kwa ndege”

Hii imefanya iwe vigumu sana kumtoa nchini kwa matibabu ya hali ya juu. kwa kuwa hakuna shirika la ndege litakalomsafirisha..

Baba kwa sasa amelazwa katika hospitali moja kubwa na bora zaidi tuliyopata nchini Nigeria kuanzia leo na hospitali hiyo imempatia jopo la wataalamu wa hali ya juu sana.

Baba anapata nafuu tunawasihi marafiki zake, wafanyakazi wenzake, mashabiki na Wanaijeria kwa ujumla wamweke katika sala zao na kutokutangaza ripoti ambazo hazijathibitishwa kuhusu afya ya baba yetu.

Asanteni Wanaijeria, wote mmekuwa mkituunga mkono sana kipindi hiki. Mungu awabariki ninyi nyote.

Valatine Okafor

Kwa niaba ya Familia….”

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.