Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kuota vipele kwenye mashavu ya uke

Kuota vipele kwenye mashavu ya uke

vipele kwenye mashavu ya uke huweza kusababishwa na sababu nyingi mbali mbali ikiwemo matatizo ya ngozi,maambukizi ya magonjwa n.k,

Na Dawa ya vipele kwenye mashavu ya uke hutegemea na chanzo husika cha tatizo hili. Katika Makala hii tunajadili Zaidi kuhusu tatizo la Kuota vipele kwenye mashavu ya uke, chanzo chake,dalili pamoja na Tiba yake.

Dalili za vipele kwenye mashavu ya uke

Kwa kawaida dalili za vipele kwenye mashavu ya uke huambatana na muwasho wa mara kwa mara, na hali hii ya muwasho huzidi kuongezeka au kuwa mbaya Zaidi pale unapojikuna eneo husika.

Kwa Ujumla dalili za vipele kwenye mashavu ya uke ni pamoja na;

  • Kupata muwasho au kuhisi kuungua sehemu ya upele kuota
  • Kutokea kwa vipele vinavyoonekana kwa macho
  • Kuwa na malengelenge au vidonda
  • Ngozi kuwa na mabaka mabaka
  • Kuvimba kwa ngozi
  • Wengine hupata homa

vipele kwenye mashavu ya uke huweza kuambatana pia na;

– Uchafu wenye harufu mbaya kutoka ukeni

– Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa n.k

Chanzo cha vipele kwenye mashavu ya uke

Asilimia kubwa tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke ni tatizo ambalo hutibika na husababishwa na sababu za kawaida, Ingawa wakati mwingine huweza kuwa tatizo Sugu na ambalo halitibiki kulingana na chanzo chake.

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za vipele kwenye mashavu ya uke;

1. Matatizo ya Ngozi kama vile Contact dermatitis,

Tatizo hili la ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayosababisha vipele kwenye mashavu ya uke kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya Tafiti za Mwaka 2014 zilionyesha Contact dermatitis huhusika na tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke kwa karibu asilimia 50% ya wanawake wenye shida hii.

2. Tatizo la kuvimba kwa Uke au mashavu ya Uke(Vaginitis au vulvovaginitis),

kwa mujibu wa vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa “the Centers for Disease Control (CDC)”, moja ya chanzo kikubwa cha tatizo hili ni maambukizi ya bacteria au fangasi.

3. Maambukizi ya Fangasi-Yeast infections (Candida),

Watu wengi wenye vipele kwenye mashavu ya uke pia hutokana na maambukizi ya fangasi sehemu za siri hasa fangasi ambao hujulikana kama Candida albicans.

4. Magonjwa ya Zinaa kama vile Trichomoniasis (trich),

ugonjwa huu hudababishwa na protozoan parasite na husambazwa kwa njia ya kujamiiana.

Tiba ya Trichomoniasis ni pamoja na matumizi ya antibiotics kama vile metronidazole (Flagyl) au tinidazole (Tindamax).

5. Tatizo la Psoriasis

Psoriasis ni tatizo kwenye mfumo wa kinga ya mwili(autoimmune condition) ambalo matokeo yake huathiri ngozi ikiwemo ngozi ya Sehemu za Siri.

Tatizo hili huweza kuwa chanzo cha vipele kwenye mashavu ya uke au vidonda(Psoriasis lesions),

Lakini tatizo hili la Psoriasis haliwezi kuathiri sehemu ya ndani ya Uke.

6. Maambukizi ya Virusi- Molluscum contagiosum

Molluscum contagiosum ni maambukizi ya Virusi ambayo kwa asilimia kubwa hushambulia ngozi, maambukizi haya huweza kusambaa kwa njia ya kujamiiana n.k,

Moja ya dalili zake ni kusababisha upele(bumps) wenye ukubwa wa millimeters kati ya 2 mpaka 5 (mm).

7. Ugonjwa wa Scabies

Moja ya dalili kubwa za ugonjwa wa Scabies ni kusababisha vipele kwenye ngozi ambavyo huweza kuambatana na muwasho,

Hivo wanawake wenye ugonjwa wa Scabies huwezs kupata tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke.

8. Kuwa na Chawa Sehemu za Siri(Pubic lice)

Chawa Sehemu za siri(Pubic lice) ni wadudu jamii ya parasite wadogo sana ambao huweza kuathiri nywele za Sehemu za Siri na chakula chao kikubwa ni damu ya binadamu.

Unaweza kuwapata baada ya kujamiiana na mtu mwenye hawa chawa, au kupitia nguo,mashuka,taulo za kuogea n.k kutoka kwa mtu mwenye chawa.

Wadudu hawa huweza kusababisha hali ya muwasho sehemu za Siri na eneo la mashavu ya Uke kwa ujumla.

Chawa Sehemu za Siri(Pubic lice) huweza kutibiwa na dawa kama vile permethrin (Nix).

9. Maambukizi ya Genital herpes

Genital herpes husababishwa na Virusi vinavyojulikana kama herpes simplex virus, hasa hasa aina ya 2 (HSV-2).

Huu ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa yanayoenezwa kwa kiasi kikubwa, na asilimia kubwa dalili zake huchukua siku 4 mpaka 7 kuanza kuonekana toka siku ya kuambukizwa.

Dalili zake ni pamoja na kuwa na vipele, malengelenge au vidonda vyenye maumivu pamoja na kuhisi hali ya kuungua sehemu za Siri, kuzunguka uke, kwenye matako, na sehemu ya haja kubwa.

10. Ugonjwa wa Kaswende(Syphilis)

Kaswende ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na bacteria Treponema pallidum. Ugonjwa huu pia huweza kusababisha vipele kwenye mashavu ya uke au vidonda ambazo hujulikana kama chancre.

11. Tatizo la masundosundo(Genital warts)

Tatizo hili ni miongoni mwa magonjwa ya Zinaa ambapo chanzo chake ni maambukizi ya human papillomavirus (HPV).

Pia tatizo hili huweza kusababisha vipele kwenye mashavu ya uke.

Hizo ndyo baadhi ya Sababu za Mwanamke kupata Tatizo la vipele kwenye mashavu ya uke.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.