Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

kunywa dawa na maziwa

kunywa dawa na maziwa

Dawa ambazo haziruhusiwi kuchanganya na maziwa

Fahamu kwamba; Maziwa yanaweza kuingiliana na jinsi madini chuma yanavyofyonzwa tumboni, na kalsiamu inayopatikana katika bidhaa za maziwa inaweza kuzuia mwili kunyonya antibiotics/viuavijasumu vya tetracycline na ciprofloxacin pamoja na dawa za matatizo ya tezi, kwa hivyo utapata chini ya kiwango katika mwili wako.

Haya hapa ni maelezo kuhusu dawa ambazo haziruhusiwi kuchanganywa na maziwa;

1. Dawa Za Tezi la Shingoni(Thyroid Medication)

Watu wengi hutumia dawa za kutibu matatizo ya tezi kama vile tatizo la hypothyroidism, Tatizo ambalo huhusisha tezi hili la shingoni kutokufanya kazi vizuri na kuzalisha kiwango cha kutosha cha vichocheo vinavyojulikana kama thyroid hormone.

Zipo baadhi ya dawa za kutibu tatizo hili ambazo haziruhusiwi kutumika pamoja na maziwa, dawa hizo ni pamoja na;

  • levothyroxine (Synthroid, Levoxyl, Unithroid, Levothroid),
  • Armor Thyroid,
  • liothyronine (Cytomel).
  • Pia Levothyroxine pamoja na liothyronine huweza kupatikana kwenye kidonge kimoja(one tablet).

Dawa zote za tezi la shingoni(thyroid medications) unashauriwa kutumia tumbo likiwa halina kitu, lakini dawa jamii ya Levothyroxine, hii imeonekana zaidi kuingiliana na maziwa au bidhaa za maziwa hali ambayo inaathiri ufyonzwaji au kupelekea zifyozwe kwa kiwango kidogo sana mwilini.

2. Dawa jamii ya Antibiotics

Kuna antibiotics nyingi ambazo hazipaswi kutumiwa pamoja na Maziwa au bidhaa za maziwa kwa sababu kalsiamu katika Maziwa inaweza kupunguza kiasi cha dawa ambazo mwili wako unaweza kutumia.

Mfano wa dawa hizo ni pamoja na;

  • Dawa jamii ya Tetracycline,
  • minocycline
  • doxycycline.

Ili kuepuka kuingiliana, unashauriwa kutumia dawa kama vile tetracyclines angalau kabla ya saa moja ndipo utumie maziwa/bidhaa zenye maziwa au utumie dawa hizi masaa mawili baada ya kutumia maziwa au bidhaa za maziwa.

Dawa zingine ni jamii ya Fluoroquinolone, kama vile;

  •  ciprofloxacin (Cipro),
  • levofloxacin (Levaquin), and
  • Pamoja na moxifloxacin (Avelox).

Kama vile mwingiliano wa maziwa na tetracyclines, matokeo sawa hutokea na kwenye dawa jamii ya fluoroquinolones. Tena, hii ina maana kwamba maambukizi yako yanaweza yasitibiwe kwa ufanisi au kikamilifu. Hii inaweza kufanya vijidudu kuwa vigumu zaidi kutibu katika maambukizo yajayo.

Unashauriwa kutumia dawa jamii ya fluoroquinolones angalau kabla ya masaa mawili ndipo utumie maziwa/bidhaa zenye maziwa au utumie dawa hizi masaa manne baada ya kutumia maziwa au bidhaa za maziwa.

3. Virutubisho vyote vyenye madini chuma(Iron Supplements)

Baadhi ya watu hutumia virutubisho vyenye madini ya chuma kwa tatizo la upungufu wa damu(anemia), hali ambayo damu yako haina chembechembe nyekundu za damu za kutosha(red blood cells).

Mfano wa dawa hizo ni pamoja na;

  • Dawa za Fefol, vidonge vya kuongeza damu kwa Mjamzito
  • ferrous sulfate
  • Pamoja na ferrous gluconate.

Kalsiamu katika bidhaa za maziwa inaweza kuzuia mwili kunyonya madini chuma ya kutosha kutoka kwenye dawa zako. Ndiyo maana inapendekezwa subiri angalau saa 2 baada ya kula bidhaa za maziwa kabla ya kutumia kirutubisho chako cha madini ya chuma.

Uchunguzi unaonyesha kuwa madini chuma hutumika vizuri zaidi kwenye tumbo ambalo halina kitu kwa sababu yatafyonzwa vizuri kwa njia hiyo.

Wakati mwingine, virutubisho vyenye madini chuma husababisha athari zisizofurahisha, kama vile tumbo kuuma n.k. Katika kesi hiyo, ni vizuri kuchukua ziada na chakula kidogo, lakini hakikisha kuwa sio chakula chenye maziwa kwa sababu kalsiamu ndani yake inaweza kuingiliana.

4. Dawa za matatizo ya mifupa kama vile Osteoporosis Medication

Osteoporosis ni hali inayotokea kwa watu wazee, hasa wanawake, ambapo mifupa yao hukonda na kuwa tete au dhaifu sana. Hatari ya kuvunjika mfupa huongezeka ikiwa una tatizo la osteoporosis. Dawa zinazoitwa bisphosphonates zimewekwa ili kuimarisha mifupa.

Maziwa,bidhaa za maziwa au vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Calcium huweza kuathiri ufyonzwaji wa dawa hizi, hali ambayo husababisha dawa hizi kufyozwa katika kiwango kidogo na hivyo kutumika katika kiwango kidogo zaidi mwilini.

Mfano wa dawa hizo ni pamoja na;

  • Actonel (risedronate),
  • Fosamax (alendronate),
  • Pamoja na Boniva (ibandronate).

Ikiwa unatumia dawa hizi, hakikisha unasubiri saa kadhaa kabla ya kunywa maziwa au kula bidhaa nyingine za maziwa,

Dawa kama vile Bisphosphonates kwa kawaida unashauriwa kutumia asubuhi kabla hujala chochote( tumbo likiwa halina kitu),

Ukiwa unatumia dawa za alendronate pamoja na risedronate, unahitaji kusubiri angalau dakika 30 baada ya kutumia dawa kabla ya kutumia bidhaa zozote za maziwa,

Na Ukiwa unatumia ibandronate za kunywa unahitaji kusubiri angalau dakika 60.

5. Dawa jamii ya Lithium

Dawa jamii ya Lithium salts hutumika kwa watu wenye matatizo kama vile bipolar disorder, matatizo yanayohusu afya ya akili(psychiatric illnesses) kama vile depression pamoja na schizophrenia.

Pia hushauriwi kuchanganya dawa hizi pamoja na maziwa au bidhaa za maziwa,

Ikiwa unatumia dawa hizi, hakikisha unasubiri saa kadhaa kabla ya kunywa maziwa au kula bidhaa nyingine za maziwa.

6. Dawa za Virusi vya Ukimwi(HIV Medication)

Moja ya dawa zinazotumika kwa wagonjwa wenye VVU ni pamoja na Dovato na Tivicay (dolutegravir),

dawa hizi hutumika zikiwa vimeunganishwa pamoja na dawa zingine za Ukimwi.

Na wakati mwingine dawa za dolutegravir hutumika kama kinga(prophylactic) ili kuzuia maambukizi kwa mtu ambaye amekuwa kwenye mazingira hatarishi ya kupata VVU.

Kutumia dolutegravir na virutubisho vya kalsiamu ni sawa ikiwa imechukuliwa pamoja na chakula. Vinginevyo, mwingiliano huu unaweza kusababisha ufyozwaji wa chini wa dawa hizi.

Kuchanganya vitu hivi viwili kunaweza kusababisha kupungua kwa viwango vya dawa kwenye damu, Inapendekezwa kuchukua dolutegravir masaa mawili kabla au saa sita baada ya kutumia vyakula au virutubishi vyenye kalsiamu.

Hitimisho:

Hizo ndyo baadhi ya Dawa ambazo haziruhusiwi kuchanganya na maziwa.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.