Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Jokofu la nyumbani latumika kuhifadhi dawa

Jokofu la nyumbani latumika kuhifadhi dawa

Zahanati ya Kijiji cha Itumba Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, haina jokofu maalumu la kuhifadhia dawa zinazotumika kutibu binadamu, badala yake inatumia la mahitaji ya nyumbani kuweka dawa ili zisiharibike.

Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Luganuza Damas alisema hayo jana, wakati akitoa taarifa za utoaji huduma kwa Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka baada ya kutembelea zahanati hiyo.

“Licha ya ukosefu wa jokofu, pia kuna changamoto kunapojitokeza dharura kwa wajawazito nyakati za usiku, wataalamu wanaishi mbali na kituo cha kazi kufuatia kutokamilika kwa nyumba ya watumishi,” alisema Damas.

Akizungumzia kitendo cha kuhifadhi dawa kwenye majokofu ya kawaida, Mtaalamu wa Famasia, Hamis Msagama alisema kama jokofu haliwezi kupoza kwa kiwango stahiki ni tatizo.

“Kwa hapo ni kuangalia aina ya dawa na aina ya friji linalotumika, kama haliwezi kupoza kwa kiwango stahiki ni shida, dawa zimeandikwa hapo kwenye lebo na ubaridi unaohitajika,” alisema Msagama.

Akizungumzia kutokuwapo nyumba za watumishi hao karibu, Dk Luganuza alisema wakati mwingine wanashindwa kufika kwa wakati kunapokuwa na dharura ili kuwasaidia wajawazito, hali inayochangui kujifungua bila usaidizi wa wataalamu.

“Tunaomba Serikali isikie kilio chetu angalau tupate jokofu dogo na kukamilisha nyumba ya watumishi ili kutuondoa kwenye mazingira magumu ya utendaji wa kazi wanayopitia,” alisema.

Diwani wa Chalangwa, Haji Elius aliiomba Serikali kuharakisha ujenzi ya nyumba ya watumishi ili kuboresha huduma za afya kwa jamii na kunusuru vifo visivyo vya lazima.

“Kwa kweli tuombe Serikali kuona umuhimu kuboresha huduma sambamba na kujenga nyumba za watumishi ili kuwasaidia kufanya kazi kwa weledi mkubwa katika kutoa huduma, hususan kuokoa maisha ya wajawazito wakati wa kujifungua,” alisema Diwani Elius.

Mkazi wa Chalangwa, Janeth Ndomba aliitaka Serikali ione umuhimu wa kuharakisha ujenzi wa nyumba za watumishi ili wafanye kazi jirani na kituo cha kazi.

Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka alisikitishwa na ukosefu wa jokofu katika zahanati hiyo na kuahidi kufuatilia kwa haraka.

Mwananchi ilipomtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Timamu Kambona kujua halmashauri imejipangaje kutatua changamoto hiyo, simu yake iliita bila kupokewa, huku wasaidizi wake wakieleza yuko katika safari ya kikazi.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.