Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Vifo vya watoto chini ya miaka 5 vimepungua kutoka 67 hadi 43

VIFO VYA WATOTO CHINI YA MIAKA 5 VIMEPUNGUA KUTOKA 67 HADI 43 KWA KILA VIZAZI HAI 1,000 MWAKA 2022

Na. WAF – Dar es Salaam

Vifo vya watoto wa umri chini ya miaka Mitano vimepungua kutoka vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2016 mpaka vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000 2022.

Waziri Ummy amesema hayo Januari 10, 2024 akinukuu taarifa ya afya ya uzazi mama na mtoto na viashiria vya Malaria ya Mwaka 2022 wakati akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za Afya nchini kwa mwaka 2023.

Amesema, mafanikio hayo ya kupunguza vifo hivyo yametokanana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.

Waziri Ummy amesema vyumba vya uangalizi maalumu vinavyohudumia watoto wachanga walio mahututi (Neo natal Care units) vimeongezeka kutoka Hospitali 125 mwaka 2022 hadi Hospitali 189 mwaka 2023.

“Tukirudi nyuma kidogo kwa mwaka 2018, Tanzania ilikuwa na NICU 14 tu na hii ina maana nchi ilikuwa na ombwe kubwa la huduma za Afya kwa watoto wachanga na hivyo watoto wengi kufariki kwa kukosa huduma stahiki.” Amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy amesema vituo vinavyofanya upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni vimeongezeka kutoka 388 Mwaka 2022 hadi kufikia Vituo 523 Mwaka 2023 lengo ni kuhakikisha tunatoka maisha ya watoto wachanga.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.