Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA KUPOTEA KWA NYWELE(TRACTION ALOPECIA),CHANZO,DALILI NA TIBA

TATIZO LA KUPOTEA KWA NYWELE(TRACTION ALOPECIA),CHANZO,DALILI NA TIBA

TRACTION ALOPECIA ni tatizo ambalo huhusisha mtu kupotea kwa nywele zake au nywele kunyonyoka zenyewe kutokana na kuvutwa sana mara kwa mara,mfano;

kwa wadada wanaosuka,wanaoweka nywele dawa,wanaotumia mitindo ya kuchoma nywele au wanaobana sana nywele kwa mitindo tofauti tofauti. Tatizo hili huweza kuisha endapo umeacha kufanya vitu hivi ambavyo vinasababisha nywele kupotea.

DALILI ZA TATIZO HILI LA NYWELE KUPOTEA(TRACTION ALOPECIA)

– Kuanza kama kichunusi eneo la kichwani ambapo nywele zimeota,kisha kuendelea taratibu

– Kuweka wekundu kwenye baadhi ya maeneo ya ngozi kichwani

– Kuhisi Hali ya kuwashwa sana kichwani mara kwa mara

– Ngozi ya kichwani kuanza kuwa na vidonda mithili ya mapunye

– Ngozi ya kichwani kutoka kama magamba

– Shida ya folliculitis (inflammation of the hair follicles) n.k

CHANZO CHA TATIZO LA NYWELE KUPOTEA AU KUTOKA (TRACTION ALOPECIA)

Chanzo kikubwa cha shida hii,ni nywele kuvutwa sana,hali ya kuvutwa sana nywele mara kwa mara hupelekea nywele kulegea na kuachia kwenye vishikizo vyake(follicle). Mfano;

✓ Kwa wadada wanaosuka nywele zao

✓ Wanaobana sana nywele kwa vibanio na mitindo mbali mbali

✓ Wanaounguza nywele

✓ Wanaoweka nywele dawa mara kwa mara n.k

✓ Mitindo ya nyweke kama dreadlocks n.k

✓ Kuvaa mawigi au Weaves kwa muda mrefu sana

JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI LA NYWELE KUTOKA

– Badilisha mitindo ya nywele na kutumia mitindo ambao sio yakubana sana nywele

– Epuka mitindo ya kuweka nywele dawa

– Epuka kuvaa mawigi au weaves kwa muda mrefu

– Epuka matumizi ya hair relaxers

– Usilale na Roller kichwani,chanua tu nywele zako

– Hakikisha moto wa kwenye drayer unakuwa mdogo mno wakati wa kukausha nywele n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Kama umefanya vitu vyote hivo lakini bado tatizo lipo unaweza kukutana na wataalam wa ngozi yaani dermatologist,kisha watafanya vipimo zaidi kama kuchukua Biopsy ili kuangalia chanzo cha tatizo na kukupa tiba,

pia kuna matibabu mengine kama vile matumizi ya dawa jamii ya;

– Antibiotics, ili kuzuia maambukizi ya bacteria kwenye vidonda

– Matumizi ya topical steroids, ili kuondoa uvimbe wowote kichwani

– Matumizi ya dawa za fangasi kama vile antifungal shampoos n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.