Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA SITAKI (PSITACOSSIS),CHANZO,DALILI NA TIBA

UGONJWA WA SITAKI (PSITACOSSIS),CHANZO,DALILI NA TIBA

Hii ni homa ambayo huwapata binadamu itokanayo na kuambukizwa vimelea wa chlamydia psittaci ambae hupatikana kwa kuku,bata,kanga na ndege wengine. Ugonjwa huu upo sana lakini cha ajabu watu wengi bado hawaujui au kuutilia maanani.

Ugonjwa huu hupelekea watu kupata matatizo ya kifua(homa ya mapafu,pneumonia),mafua,kukohoa nk ambayo watu wengi huchukulia ni homa za kawaida

Kimelea wa sitaki huishi kwa ndege kama kuku na ni hutolewa kwenye vinyesi vya ndege hao au majimaji yao,hivo basi vimelea hawa humuingia mtu pale ambapo mtu husika amekua karibu na maeneo yenye kuku wenye huu ugonjwa kwa maana kwenye mabanda yao na kuvuta yale mavumbi vumbi yaliyopo kwenye mabanda yao,

kama kuku hao walikua na ugonjwa wa sitaki na mtu akavuta hayo mavumbi basi anaweza kupata maambukizi ya sitaki,binadamu kwa binadamu ni ngumu sana kuambukizana

DALILI ZA UGONJWA WA SITAKI

Mara baada ya binadamu kupata kimelea wa ugonjwa wa sitaki na kuingia mwilini mwake basi ataanza kuona dalili ndani ya siku 5 hadi 15. Kama unafanya kazi zinazohusu aidha ufugaji wa kuku au kuuza kuku na ukawa na dalili zifuatazo basi jua kwamba una uwezekano ukawa na ugonjwa wa sitaki

?Homa kali za ghafla (fever of abrupt onset)

?Maumivu makali ya kichwa(headache)

?Kikohozi kikavu(dry cough)

?Maumivu ya kifua(chest pain)

?Kifua kubana na kuishiwa pumzi(dyspnea)

?Kukohoa damu(hemoptysis)

?Maumivu ya misuli(myalgia)

?Madonda kooni na koo kuwasha(pharyngitis)

?Kuharisha(diarrhea)

MATIBABU YA UGONJWA HUU WA SITAKI

Ugonjwa huu unatibika vizuri kabisa kama ukigundulika haraka na kupata dawa sahihi
Kwa wataalam wa afya, kama mgonjwa anafanya kazi za kuku,bata,kanga n.k na anapata dalili tajwa hapo juu basi waza pia ugonjwa wa sitaki ili mgonjwa apate dawa sahihi

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.