Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Binti ajinyonga baada ya kugombezwa na baba yake

Binti ajinyonga baada ya kugombezwa na baba yake

Kahama. Mariamu Ngasa (28) mkazi wa Mtaa wa Nyihogo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kitenge, baada ya kugombezwa na baba yake kwa kutoroka na kwenda kwa mchumba wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano,  Januari 24, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akieleza kuwa chanzo ni kugombezwa.

 “Mtoto akikosea lazima agombezwe, niwaombe wazazi tuwe makini katika malezi, watoto wamekuwa na kiburi, wanakanywa lakini hawaelewi na wengine wanaona wameonewa. Nawaombeni pia muwashirikishe viongozi wa dini, kimila na walimu katika malezi” amesema.

Akizungumza na waandishi wa habari, mama mlezi wa marehemu, Mariamu William amesema, binti yake alikwenda eneo la Mwime lenye wachimbaji wadogo wa madini kuuza vitumbua, lakini hakurudi nyumbani hali iyozua wasiwasi na kuanza kumtafuta pasipo mafaniko.

Amesema baada ya siku saba alirejea nyumbani Januari 18,2024 akiwa na fedha za mauzo ya vitumbua mkononi ndipo baba yake alipomuuliza alikokuwa na alijibu kuwa alikutana na mpenzi wake aliyemzalisha mtoto wa kwanza na ndiye aliyemrubuni kwenda naye nyumbani kwake.

“Binti yangu alizalia nyumbani mtoto wake wa kwanza kitendo ambacho sisi kama wazazi kilituumiza, kwani hata huyo mwanaume aliyemzalisha hakuwahi kufika nyumbani ili kumtambua, hivyo baba yake aliingiwa na wasiwasi huenda akapata mimba nyingine,” amesema mama mlezi wa marehemu.

Amesema baada ya kula chakula cha mchana, aliingia chumbani kwake na kufunga mlango na baada ya muda mfupi, walipokwenda kumwangalia walikuta amejinyonga kwa kutumia kitenge.

Kwa upande wake baba yake Mariamu, Robert Ngasa amesema, Januari 18,2024 mwaka huu alimhoji mwanawe kuhusu kutoweka kwake nyumbani kwa wiki moja na alikiri kwenda kwa mchumba wake ambaye alimuahidi angekwenda kujitambulisha Februari mwaka huu.

“Ni kweli nilimgombeza kwa kitendo alichofanya lakini sikumpiga kwa sababu aliomba radhi na kusema mchumba wake angekuja kwangu Februari.

“Baada ya hapo niliondoka nikaenda kazini baada ya muda nikapewa taarifa za kujinyonga kwa mwanangu,” amesema Ngasa.

Via:Mwananchi.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.