Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA UGONJWA WA PELLAGRA

DALILI ZA UGONJWA WA PELLAGRA

Ugonjwa wa pellagra kama nilivokwisha kusema hapo awali ni kwamba unaleta matatizo katika mfumo wa fahamu,mfumo wa mmengenyo wa chakula na ngozi hivo basi dalili zake hua zinajikita sana kwenye mifumo hiyo; Dalili kuu za ugonjwa huu ni:

1) Matatizo ya ngozi: mgonjwa wa pellagra atakua na ngozi ngumu,nyeusi,inayowasha hasa nyakati za kiangazi na vipindi vya jua kali;

mabadiliko hayo kwenye ngozi hua sana kwenye shingo (Casal’s “necklace),kifuani kwa juu,mgongoni kwa juu,mikono yote miwili hasa hasa kwenye viganja kwa nyuma,miguuni (kwa wale wasiovaa suruale) na vinapokua vinaanza vinauma lakini kadiri muda unavozidi kwenda vinakua haviumi wala haviwashi.

Matatizo au mabadiliko ya ngozi kama yakikaa muda mrefu bila kutibiwa basi ngozi huzidi kua ngumu,kua rafu,nyeusi sana nay a kutisha,ngozi hua kama ya bata maji (goose skin)

2) Kuharisha tena kuharisha sana (Diarrhea)

3) Kua na Imani mbaya na potofu juu yako mwenyewe au vitu vinavokuzinguka (Delusional disorder)

4) Kuogopa ogopa mwanga (photophobia)

5) Usahaulifu usio wa kawaida hata kama mtu hajazeeka (Dementia)

6) Kukosa usingizi,kukosa raha ya kila kitu,kupoteza tumaini la kila kitu (depression)

7) Maumivi ya kichwa mara kwa mara (reccurent headache)

8) Kua na hisia,kusikia sauti au kuona vitu ambavyo havipo (Hallucinations) yaani unakuta mtu amekaa mwenyewe lakini anapiga stori kana kwamba yuko na kikundi cha watu

9) Utapiamlo kwa sababu ya kutokula ,kuharisha sana na kupoteza virutubisho vingi (malnutrition and eventually cachexia)

10) Mwili kuchoka choka mara kwa mara

11) Kua na uwezo mdogo wa kuelewa mambo au kupungua kwa umakini (poor concentration)

12) Kupoteza au kupungua hamu ya kula (poor appetite)

13) Maumivu ya tumbo,tumbo kuvuruga vuruga (epigastric discomfort and abdominal pain)

14) Kua na msongo wa mawazo na hasira hasira sana (irritabil-ity and anxiety)

15) Kuchanganyikiwa kwa kuanza kupiga watu,kukosa aibu nk (psychosis)

16) KIFO (DEATH)

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.