Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI

MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI

Moyo kushindwa kufanya kazi ni ugonjwa utokanao na kuharibika kwa muundo au utendaji kazi wa moyo. Hali hii inaweza pelekea moyo kushindwa kusukuma damu kupeleka maeneo mbalimbali ya mwili.

Ugonjwa wa moyo ni miongoni mwa sababu za vifo vingi kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Miongoni mwa vihatarishi ni kufata mfumo wa maisha wa mataifa ya magharibi.

SABABU ZINAZOPELEKEA MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI

Sababu hizi zimegawanywa kitaalamu katika makundi mbalimbali. Nazo ni

1. Shida katika mshipa ya damu inayosambaza damu kwenye moyo

2. Shinikizo la juu la damu

3. Kuongezeka kwa ukinzani katika mishipa ya damu

4. Kuharibika kwa vali za moyo

5. Kuwepo kwa matundu au njia zinazopelekea damu kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine

6. Matatizo sugu ya mapafu

7. Matatizo ya misuli ya moyo

8. Kuzeeka

9. Upungufu wa damu mwilini

10. Upungufu wa vitamin na virutubisho

11. Matatizo/ magonjwa yahusuyo homoni

12. Matatizo ya mdundo na kiwango cha mapigo ya moyo. Nk

ALAMA NA DALILI ZA SHIDA YA MOYO

1. Mwili kuchoka

2. Kukosa hewa au kupumua kwa shida hasa pale mtu anapofanya kiwango flani cha kazi, anapolala chali na hata kukosa hewa kabisa wakati wa usiku kunakoambatana na kukohoa

3. Kutuama kwa maji mwilini kama miguuni na kwenye mapafu n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.