Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

CHANZO CHA TATIZO LA TUMBO KUZALISHA KIWANGO KIKUBWA CHA ACID

 TUMBO

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA TUMBO KUZALISHA KIWANGO KIKUBWA CHA ACID


Tatizo la uzalishaji wa kiwango kikubwa cha acid tumboni au gastric Acid ni tatizo ambalo huweza kumpata mtu yoyote na kuleta madhara makubwa sana mwilini.


CHANZO CHA UZALISHAJI WA KIWANGO KIKUBWA CHA ACID TUMBONI


Chanzo kikubwa ni kuzalishwa kwa kiwango kikubwa cha hormone ambayo hujulikana kama GASTRIN,


Hormone hii ndyo inatoa taarifa kuhusu kiwango cha uzalishaji wa acid tumboni yaani Gastric acid.


Uzalishwaji wa kichocheo hiki cha GASTRIN kupita kiasi huchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;


– Maambukizi ya Bacteria kama HELICOBACTER PYLORI


– Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo hupunguza kiwango cha acid tumboni


– Tatizo la Zollinger-Ellison syndrome


– Tatizo sugu la Figo kufeli yaani Chronic Kidney failure


– Njia ya kutoka tumboni kwenda kwenye utumbo mdogo kuziba

N.k


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


✓ maumivu makali ya tumbo hasa ukiwa na Njaa


✓ tumbo kujaa gesi mara kwa mara


✓ kuhisi kichefuchefu na kutapika


✓ Uzito wa mwili kushuka kwa kasi sana


✓ Hamu ya chakula kupotea kabsa


✓ Kupata tatizo la kiungulia au Heartburn mara kwa mara


MADHARA YAKE


tatizo hili huweza kusababisha madhara mbali mbali kama vile;


– Mtu kuwa na vidonda vya tumbo


– Tatizo la kuvuja damu ndani ya tumbo

N.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


Tatizo hili hutibika kwa kutumia dawa mbali mbali kama vile; Omeprazole, na aina nyingine za antibiotics, pia mgonjwa hupewa dawa mbali mbali za kudhibiti dalili kama vile; Kichefuchefu,kutapika,kiungulia,n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.