Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mwanaume kuchelewa kukojoa,Chanzo chake hiki hapa,Soma kufahamu(delayed ejaculation)

Mwanaume kuchelewa kukojoa,Chanzo chake hiki hapa,Soma kufahamu(delayed ejaculation)

Mwanaume kuchelewa kukojoa; huhusisha pale ambapo mwanaume anakumbwa na tatizo la kushindwa kumwaga baada ya kufanya mapenzi hali ambayo humchukua muda kuliko kawaida.

Baadhi ya wanaume wenye kuchelewa kukojoa wanahitaji dakika 30 au zaidi za kusisimuliwa kimapenzi ili kuwa na mshindo na kumwaga. Wanaume wengine huenda wasiweze kumwaga kabisa (anejaculation).

Lakini, hakuna Muda maalum ambao unaonyesha utambuzi wa kuchelewa kukojoa au kumwaga. Badala yake, pengine unakabiliwa na kukojoa kwa kuchelewa ikiwa kuchelewa kunasababisha uwe na Msongo wa mawazo au kufadhaika,ikiwa unapaswa kuacha kufanya mapenzi kwa sababu ya uchovu, hasira,kupoteza hamu ya tendo, Uume kushindwa kusimama au ombi kutoka kwa mpenzi wako.

Mwanaume kuchelewa kukojoa; pia hujulikana kama mwanaume kuchelewa kufika Mshindo(Delayed ejaculation/delayed orgasm) Na hutokea unapochukua muda mrefu na kuhitaji msisimko mwingi ili kufikia kileleni na kutoa shahawa, na Katika baadhi ya matukio, huenda usimwage kabisa.

Tatizo la Mwanaume kuchelewa kukojoa linaweza kuwa tatizo la muda mfupi tu au tatizo la kudumu. Ni kawaida kwa baadhi ya Vipindi Kwa Mwanaume kuchelewa kukojoa, ingawa ikiwa ni tatizo endelevu na la kukupa mawazo unahitaji Tiba.

Dalili za tatizo la Mwanaume kuchelewa kukojoa

Baadhi ya wanaume wenye kuchelewa kukojoa wanahitaji dakika 30 au zaidi za kusisimuliwa kimapenzi ili kuwa na mshindo na kumwaga. Wanaume wengine huenda wasiweze kumwaga kabisa (anejaculation).

Lakini, hakuna Muda maalum ambao unaonyesha utambuzi wa kuchelewa kukojoa au kumwaga. Badala yake, pengine unakabiliwa na kukojoa kwa kuchelewa ikiwa kuchelewa kunasababisha uwe na Msongo wa mawazo au kufadhaika,ikiwa unapaswa kuacha kufanya mapenzi kwa sababu ya uchovu, hasira,kupoteza hamu ya tendo, Uume kushindwa kusimama au ombi kutoka kwa mpenzi wako.

Mara nyingi, wanaume wanaweza kuwa na shida ya kufikia mshindo wakati wa tendo la ndoa au shughuli zingine za ngono na wenzi wao. Wanaume wengine wanaweza kutoa manii tu wakati wa kupiga punyeto.

Tatizo la Mwanaume kuchelewa kukojoa limegawanyika kwenye aina mbali mbali ikiwemo;

1. Lifelong delayed Ejaculation

lifelong delayed ejaculation, ni pale ambapo tatizo la kuchelewa kukojoa lipo kutoka unabalehe/ wakati wa ukomavu wa kijinsia.

2. Acquired delayed ejaculation

hutokea baada ya kipindi flani, wakati siku za nyuma hukuwa na shida yoyote.

3. Situational delayed ejaculation

Hapa Mwanaume anachelewa kukojoa kwa sababu ya aina ya mpenzi aliyefanya naye mapenzi, mazingira ya kufanya tendo au hali yoyote inayoweza kuathiri.(occurs only under certain circumstances).

4. Generalized delayed ejaculation

Hapa Mwanaume hachelewi kukojoa kwa sababu anafaya mapenzi na aina flani ya wapenzi au kupewa aina fulani za kusisimua, kuathiriwa na mazingira n.k.(isn’t limited to certain sex partners or certain kinds of stimulation).

Kujua aina hizi husaidia katika kugundua sababu ya msingi na kuamua ni matibabu gani yanafaa zaidi.

Chanzo cha Mwanaume kuchelewa Kukojoa

Mwanaume Kuchelewa kukojoa au kumwaga kunaweza kutokana na sababu mbali mbali iliwemo; matumizi ya baadhi ya dawa, hali fulani za kiafya sugu na upasuaji.

Au inaweza kusababishwa na matumizi mabaya ya dawa, Shida kwenye afya ya akili, kama vile kuwa na Msongo wa mawazo, wasiwasi au mfadhaiko. Mara nyingi, ni kutokana na mchanganyiko wa wasiwasi wa kimwili na kisaikolojia.

(1) Sababu za Kisaikolojia ni pamoja na;

  • Msongo wa mawazo
  • Wasiwasi
  • Huzuni
  • Woga na matatizo mengine ya afya ya akili
  • Matatizo kwenye mahusiano
  • Imani za kidini au kitamaduni pamoja na Miiko
  • Woga wa kutokufanya Vizuri kwenye tendo
  • Kutokuwa na muonekano Mzuri(Poor body image) n.k

(2) Matumizi ya baadhi ya dawa ikiwemo;

  • Baadhi ya Dawa jamii ya antidepressants
  • Baadhi ya dawa za Presha(high blood pressure medications)
  • Baadhi ya Dawa jamii ya diuretics
  • Baadhi ya Dawa jamii ya antipsychotic medications
  • Baadhi ya dawa jamii ya anti-seizure medications n.k

3. Matumizi ya Pombe

Moja ya vitu vinavyoweza kusababisha mwanaume achelewe kukoja ni pamoja na matumizi ya pombe hasa ukinywa kupita kiasi.

4. Sababu Zingine(Physical causes) ni pamoja na;

  • Kuwa na matatizo yanayoathiri mfumo wa Uzazi kwa Mwanaume
  • Kuumia eneo la Korodani au sehemu za Siri
  • Kuumia kwa Nerves eneo la Pelvic ambazo hudhibiti hali ya mwanaume kufika kileleni
  • Baadhi ya maambukizi ya magonjwa kama UTI(urinary tract infection) n.k
  • Kufanyiwa baadhi ya aina za Upasuaji wa tezi Dume(Prostate surgery), kama vile transurethral resection of the prostate or prostate removal
  • Magonjwa yanayoathiri Nerves(Neurological diseases), kama vile kisukari(diabetic neuropathy), stroke au uharibifu wa Nerves kwenye eneo la Uti wa mgongo
  • Matatizo ya Vichocheo mwilini(Hormone-related conditions), kama vile tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha vichocheo vya thyroid(hypothyroidism) au kiwango kidogo cha Vichocheo vya testosterone (hypogonadism) n.k
  • Kuwa na tatizo la Retrograde ejaculation n.k

Retrograde ejaculation; ni tatizo ambalo huhusisha mwanaume kuwa na hali ya kumwaga na mbegu kurudi kwenye kibofu cha Mkojo badala ya kutolewa nje kwenye uume.

Kwa baadhi ya wanaume, kuwa na tatizo dogo la kimwili linalosababisha kuchelewa kumwaga linaweza kusababisha wasiwasi kuhusu kumwaga wakati wa kujamiiana. Wasiwasi unaosababishwa unaweza kuzidisha tatizo la kukojoa  kwa kuchelewa.

Vitu vinavyoongeza hatari ya Mwanaume kuchelewa Kukojoa

Kuna Vitu vingi vinaweza kuongeza hatari ya Mwanaume kuchelewa kukojoa wakati wa tendo ikiwemo:

– Kuwa na Umri Mkubwa

– Kuwa na matatizo ya kisaikolojia ikiwemo;

  • Msongo wa mawazo
  • Wasiwasi
  • Woga
  • Huzuni n.k

– Kuwa na matatizo mengine ya kiafya kama vile:

  • Ugonjwa wa kisukari
  • Tatizo la multiple sclerosis n.k

– Baadhi ya matibabu kama vile baadhi ya aina za Upasuaji wa tezi dume(prostate surgery)

– Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile;

  • Baadhi ya dawa jamii ya antidepressants,
  • Dawa za Presha
  • Dawa jamii ya diuretics n.k

– Matatizo kwenye mahusiano ikiwemo;

  • Migogoro
  • Mawasiliano mabovu(poor communication) n.k

– Matumizi ya Pombe kupita kiasi n.k

Madhara ya Mwanaume kuchelewa Kukojoa

Madhara ya Mwanaume kuchelewa kukojoa wakati wa tendo ni pamoja na;

1. Kuisha kwa hamu na raha ya tendo kwako na kwa mwenza wako

2. Kujenga wasiwasi au msongo wa mawazo kuhusu utendaji wako kwenye tendo(sexual performance)

3. Kusababisha matatizo au migogoro kwenye ndoa na mahusiano hasa kwa Sababu ya kuishi maisha ya kufanya mapenzi pasipo kuridhika(unsatisfactory sex life)

4. Kutokuwa na uwezo wa kumpa Mwanamke mimba(male infertility),

Na hii hutokea Zaidi kwa wale wanaume ambao tatizo hili limefikia Hatua hawawezi kabsa kumwaga mbegu za kiume, kwa kitaalam hujulikana kama (anejaculation)

Matibabu ya Mwanaume kuchelewa Kukojoa

Matibabu ya tatizo la Mwanaume kuchelewa kukojoa hutegemea na chanzo husika, Hivo basi;

Ikiwa una tatizo la kuchelewa kukojoa au kuchelewa kumwaga au kuchelewa kufikia Mshindo hakikisha unapata Msaada kwa Wataalam wa afya au tuwasiliane hapa ndani ya @afyaclass

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass