Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kuungua na moto,Mamlaka zachunguza moto ulioteketeza bweni na kuua watoto 13

Kuungua na moto,Mamlaka zachunguza moto ulioteketeza bweni na kuua watoto 13

Yanshanpu, China/AFP. Mamlaka katika Jimbo la Henan katikati mwa China zimeanza uchunguza kuhusu chanzo cha moto uliosababisha vifo vya watoto 13 waliokuwa wamelala kwenye bweni.

Moto huo uliotokea katika Shule ya Yingcai mjini Yanshanpu, uliripotiwa kwa Idara ya Zimamoto ya eneo hilo usiku wa kuamkia Jumamosi na ulizimwa takriban dakika 40 baadaye, shirika rasmi la habari la Xinhua lilisema.

Wanafunzi 13 walifariki katika ajali hiyo, huku mtu mwingine mmoja akipata majeraha.

Makumi ya polisi walikuwa wamezingira ndani ya eneo na karibu na shule hiyo leo Jumapili asubuhi, waandishi wa habari wa AFP wameripoti.

Ofisa mmoja katika eneo la tukio ameiambia AFP kuwa “kuna uchunguzi unaendelea ndani. Hakuna mtu anayeweza kuingia.”

Madirisha kadhaa kwenye shule hiyo yalionekana yamevunjika, ikiwa ni ishara kwamba kumetokea ajali kubwa humo ndani.

Mwalimu katika shule hiyo aliliambia Shirika la Serikali la Hebei Daily kwamba waathiriwa wote walikuwa wa darasa la tatu la watoto wenye  umri kati ya miaka tisa na 10.

Siku ya Jumapili asubuhi, maduka karibu na shule yalifungwa huku zahanati ndogo katika jengo hilo ikionekana bila mtu.

Wenyeji wachache walifanya shughuli zao za siku na watoto kadhaa walikuwa wanacheza huku magari ya polisi yakizunguka eneo lililozingirwa.

Mamlaka katika eneo hilo inachunguza chanzo cha moto huo, na mtu mmoja anayehusika na shule hiyo anashikiliwa na polisi, Xinhua iliripoti Jumamosi.

Hakuna maelezo rasmi ya sababu za moto huo, ingawa baadhi ya ripoti za vyombo vya habari vya ndani zilihusiaha na hitilafu ya kifaa cha kupasha joto cha umeme.

Eneo la Yanshanpu liko nje kidogo ya Nanyang, jiji la karibu watu milioni 10, kama kilomita 850 magharibi mwa Shanghai.

Moto na ajali zingine mbaya ni mambo ya kawaida nchini China kwa sababu ya viwango duni vya usalama.

Novemba 26, mwaka jana watu 26 walikufa na kadhaa walipelekwa hospitalini baada ya moto kuteketeza ofisi ya kampuni ya makaa ya mawe katika Mkoa wa Shanxi kaskazini mwa China.

Mwezi mmoja kabla, mlipuko katika mghahawa wa nyama choma kaskazini-magharibi mwa China ulisababisha vifo vya watu 31 na kuibua kampeni ya kitaifa ya kukuza usalama mahali pa kazi.

Mnamo Aprili 2023, moto katika hospitali huko Beijing uliua watu 29 na kuwalazimu manusura waliokata tamaa kuruka kupitia madirishani kujiokoa.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass