Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Maji yanayosonga kwa kasi yamesomba makaburi katikati mwa jiji la Galkayo nchini Somalia

Maji yanayosonga kwa kasi yamesomba makaburi katikati mwa jiji la Galkayo nchini Somalia, na kuacha miili ikielea mitaani, kufuatia mafuriko mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika karne moja.

Kuonekana kwa miili iliyofukuliwa na mafuriko kumewatisha wakazi kama Ayaan Mohamed, anayeishi karibu na makaburi.

“Familia saba zikiwemo zangu zimeukimbia mtaa huo,” aliambia BBC.

Huku nyumba zikiwa zimezama kwa kiasi na mabaki ya binadamu yakielea karibu, wanahofia kuzuka kwa magonjwa, anasema.

Baadhi ya miili hiyo ilitambulika, na kuwatia kiwewe zaidi watu – na maji yanapopungua mifupa iliyofukuliwa pia huonekana.

Ayaan Mohamed anasema watu wanashangaa maiti zimesombwa kutoka kwenye makaburi yake

“Mafuriko hayo yalifichua mabaki ya mwili wa Shekhe wa Kiislamu aliyeheshimika sana. Alizikwa miaka 18 iliyopita,” Bi Mohamed anasema.

“Wanafunzi wake na mashekhe wengine walijaribu kukusanya mabaki,” alisema, lakini hawakuweza kufanya hivyo.

Haya ni matukio ambayo jiji halijawahi kushuhudia hapo awali.

Takriban watu 32 wamefariki kote nchini humo, Umoja wa Mataifa unaonya kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wanaweza kuathiriwa na mafuriko makubwa ambayo yanakuja baada ya nchi hiyo kukumbwa na ukame wa miaka mingi.

Hali ya Galkayo si mbaya kama ilivyo katika eneo la Gedo kusini mwa Somalia, ambako Mto Juba umevnja kingo zake na kusomba daraja muhimu katika mji wa Bardere.

Maji yalizidi kimo cha daraja na likaporoma a siku ya Jumamosi.

Mohamed Abdirahin anasema takriban wakazi wote wa jiji hilo wamelazimika kuhamia viungani mwake.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 70 alikuwa mfanyabiashara na mkulima aliyefanikiwa hadi wiki iliyopita wakati mafuriko yalipoharibu mali zake.

“Niliacha kila kitu nyuma,” aliambia BBC.

“Niliokoa nilichoweza kwa mikono yangu kutoka kwenye duka langu – mali nyingine zilizobaki zilisombwa na maji. Ni kana kwamba maisha yangu yaliisha hivyo,” Bw Abdirahin anasema.

Anapata ugumu wa kukubaliana na jinsi maisha yake yalivyobadilika haraka maji ya mafuriko yalipoingia dukani kwake kwanza, kisha kuangusha nyumba yake.

Bw Abdirahin pia alikuwa na shamba nje kidogo ya jiji, ambapo alienda kuangalia miti yake ya matunda iliyokomaa baada ya familia yake kulazimika kuondoka katika nyumba yao jijini.

Alikuwa akitarajia mavuno mengi mwishoni mwa mwezi wa Januari, lakini ndoto hiyo imetoweka.

“Miti ya maembe yenye urefu wa mita 10- (32ft-) ilikuwa karibu kuzama tulipokuwa tukiondoka, sikuweza kuona chochote kilichosimama kwenye ardhi yangu,” Bw Abdirahin alisema.

Source:Bbc

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass