Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA BULIMIA NERVOSA(maana yake pamoja na tabia za watu ambao wana ugonjwa huu)

 AFYA TIPS

• • • • • •

UGONJWA WA BULIMIA NERVOSA(maana yake pamoja na tabia za watu ambao wana ugonjwa huu)


Ni ugonjwa wa kisaikolojia ambao mtu anakua anakula chakula kingi kwa wakati mmoja na ambacho mtu mwingine hawezi kula kwa wakati mmoja. Wakati wa kula watu hao wanadhani hawana udhibiti wa njaa au kasi ya ulaji wao. 


Watu hao baada ya kula sana wanaanza kujihisi kwamba wamenenepa,muonekano wao umebadilika na pia wanaanza kutafuta njia za kupungua uzito kwa kujitapisha,kutafuta madawa ya kuharisha au ya kukojoa kojoa mara kwa mara


Watu hawa wanakuaga na tabia hizi baada ya kula sana


1) Kula sana/mno(Binge eating) -watu hawa wanakula chakula kingi sana ,yaani chakula cha watu watatu anawez kula mtu mmoja ndani ya muda mfupi.


2) Kutumia kinyemela madawa ya kusaidia watu wenye shida ya kupata choo ili waharishe (misuse of laxatives)


3) Kujitapisha baada ya kula (self-induced vomiting)


4) Kua na dhana ya kufunga baada ya kula sana ili


 kupunguza uzito (fasting)

5) Wanakua na ari ya mazoezi na kufanya mazoezi makali baada ya kula (excessive exercise)


6) Wanakua watu wa kujichukia juu ya unene wao,muonekano wao (Excessive concern about body weight and shape) cr:Dr.mathew


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass